Kiddle ni Google ya watoto. Yaani ni kwamba hii inafanya kazi kama Google tuu sema kilichobadilika ni kwamba hapa watoto wataonyeshwa vitu vyenye maadili tuu.
Hivi unaweza kufikiria dunia bila ya Google? – Mimi siwezi – Kumbuka Google imerahisisha vitu vingi sana kwa mfano kuna maswali unaweza ona aibu kumuuliza mtu ukaiuliza Google na ukapata majibu. Hata katika upande wa kusoma tuu zamani ili kufaulu vizuri darasani kulitokana na kusoma sana vitabu lakini sasa Google imerahisisha yote hayo.
Swali linakuja Je, kwa watoto wa kizazi hiki watatumia kweli hii?
Kusema kweli watoto au kizazi hiki cha sasa kimebadilika alafu kinajua (kinajifanya kinajua) mambo mengi sana. Sawa wana Simu janja na pengine wana uwezo mkubwa wa kutumia intaneti kuliko wazazi wao. Lakini kweli kwa motto mdogo (fikiria wa kitanzania) atakubali kutumia hii ambayo itamleta majibu ya kimaadili tuu?
Jibu hilo ukiwa nalo, Ngoja tuiangalie Kiddle!
Sasa watoto watakuwa na uwezo wa kutumia toleo lao la Google yaani Kiddle wakiwa wanatafuta vitu mbalimbali kwa kutumia njia ya utafutaji (search Engine) inayojulikana kama Kiddle.
Kiddle ina rangi maarufu ya rangi kama ile iliyopo katika nembo ya Google. Lakini katika Kiddle kampuni hilo halijatumia rangi yake nyeupe kwa nyuma (background), mbadala wake wameweka ‘theme’ ya anga (ikiwa na sayari kwa mbali) pia ikiwa na picha ya roboti
Kiddle ambayo ina sifa lukuki kama Google tuu ikiwa imepewa uwezo na Wahariri wa Google pamoja ‘Google Safe Search’ inawawezesha watoto kuweza kutafuta mambo ya kimtandao, picha , habari au hata video kwa urahisi. Pindi tuu mtoto atakapoingia katika mtandao huo (Kiddle) kama kawaida mtandao utamletea ‘link’ tofauti tofauti zinazohusiana na alichokichagua.
Katika majibu hayo, linki ya kwanza mpaka ya tatu itahusisha kurasa na mitandao salama (ya kimaadili) ambayo itakua spesheli na imechaguliwa na wahariri wa Google kwa watoto. Zinazofuata nne mpaka saba zitahusisha kurasa ambazo zimeandikwa kwa lugha nyepesi ambayo itamsaidia mtoto kuelewa bila kuwa na tatizo lolote, hizi pia zinapitiwa na Wahariri. Kuanzia majibu kutoka nane na kuendelea kurasa hizi zinakuwa zimeandikwa kwa ajili ya watu wazima lakini bado zinakuwa zimechujwa na ‘Google safe search’ japokuwa bado zinakuwa ni vigumu kidogo kwa watoto kuendana nazo
Kutokana na kwamba kurasa zitakazo kuja baada ya mtoto kutafuta kitu flani zitakuwa zimesimamiwa na zingine kuchaguliwa kabisa na wahariri na zingine zikisimamiwa na ‘Google Safe Search’ basi kaa kabisa ukijua kuwa kurasa hizo zitakuwa na mambo ya kitoto.
Ngoja Nikupe Mfano
Kwa mfano mtoto akaamua kumtafuta ‘Miley Cyrus’ kupitia Kiddle, taarifa kuhusiana na maisha yake, akaunti zake za Twitter na Instagram hazitaonyeshwa. Mbadala wake mtoto ataonyeshwa mambo ya staa huyo ya kimaadili ambayo kwa Tanzania naweza nkasema kuwa ‘Familia Nzima Inaweza Ikayaona’
Pia Kiddle haikusanyi taarifa binafsi za watoto na pia inafuta kumbukumbu zake kila baada ya masaa 24 tofauti na Google. kuingia katika mtandao huo andika www.kiddle.co