Katika siku za usoni, wananchi wa Nchi za Afrika ya Mashariki wataweza kupiga na kupokea simu bila mipaka kwa bei nafuu baada ya mashauriano ya nchi kadhaa zilizokubaliana na mpango wa One Africa Network (Mtandao mmoja wa Africa).
Shauri hilo linalounganisha nchi 11 za Africa, lilifikiwa Jumatatu ya tarehe 18 Aprili kwenye mkutano wa juu wa mawaziri wa TEHAMA na wadhibiti wa mawasiliano chini ya Smart Africa.
Nchi zinazofanya mpango huo ni Ivory Coast, Gabon, Kenya, Mali, Uganda, Senegal, South Sudan, Chad, Rwanda na Burkina Faso.
Pamoja na maendeleo mengine, mchakato wa mpango huo wa One Africa Network utafanya bei za simu na ujumbe mfupi (SMS) na pia intaneti zipugue ndani ya nchi hizo 11.
Mawasiliano hayo ya kimataifa yatapata unafuu kwenye ushuru kuwezesha mpango huu. Mawaziri wamekubaliana pia kuondoa tozo za ziada za kupokea simu za huduma ya ughaibuni(roaming charges), ikiwa ina maana msafiri kwenye hizi nchi atapaswa kulipa kama yuko nchini kwake.
Mpango huu unatazamiwa kuanza kufanyiwa kazi kuanzia mwezi Mei huku ripoti ya maendeleo ya mpango wa One Africa Network ikitazamiwa kuwasilishwa kwenye kilele cha Umoja wa Afrika mnamo mwezi Julai, Kigali Rwanda.
Dr Hamadoun Touré, mkurugenzi mkuu wa sekretarieti ya Smart Africa alisema kwamba mpango huu unatazamiwa utalisogeza bara la Afrika mbele katika kutimiza azma ya ya muungano kama ilivyowekwa na waanzilishi wa Umoja wa Afrika.
“Hakika mpango huu ni hatua ya mbele kuelekea muungano zaidi wa bara la Afrika. Ninahimiza nchi zingine za Umoja wa Afrika kujiunga na mpango huu haraka iwezekanavyo,” alisema.
“Mwisho wa siku, kuunganika kikanda ni kuleta watu pamoja na kutengeneza mazingira ya kuzalisha faida zinazoonekana na ukuaji unaomjumuisha kila nchi”
Maendeleo haya ya mpango huu yametokana na kutengenezwa kwa One Network Area kulikofanywa tayari na kanda ya juu ya nchi za Afrika Mashariki za Kenya, Uganda South Sudan na Rwanda.
Mpango wa One Network kwa Nchi za Afrika Mashariki(The East African Community One Network Area), ulioanza mwaka 2014 umepelekea ongezeko la mawasiliano na pia mapato kwa kampuni za mawasiliano. Pia, kumekuwa na ongezeko la biashara kati ya nchi hizo pamoja na kuleta wananchi karibu zaidi.
Kwenye taarifa hii, Waziri wa Vijana na TEHAMA wa Rwanda, Jean Philbert Nsengimana anakaririwa akisema kwamba mawasiliano kati ya Rwanda na Uganda yamekuwa kwa asilimia 800 huku yale ya kati ya Rwanda na Kenya yakikuwa kwa asilimia 400, huku mawasiliano kati ya Rwanda na Sudani ya Kusini yakikuwa kwa asilimia 1000!
Ingawa maendeleo ya Tanzania kujiunga na mpango wa One Africa umechukua muda mrefu, tunatazamia kujiunga karibuni.
Chanzo: newtimes.co.rw, theeastafrican.co.ke
Picha Na: theeastafrican.co.ke