Kuwekua na ukuaji wa kasi wa thamani za pesa za kidigitali – digital currency, kama vile Bitcoin. Mwanamuziki 50 Cent atengeneza mabilioni baada ya thamani ya pesa hiyo kupanda – na alikuwa ameshasahau kabisa kama anazo.
Mwaka 2014 mwanamuziki huyu alipo zindua albamu yako ya Animal Ambition alikuwa ni mwanamuziki wa kwanza kukubali mauzo ya mtandao kwa malipo ya Bitcoin. Kwa kipindi hicho alipata bitcoin 700 kupitia mauzo hayo, kwa mwaka huo bitcoin moja ilikuwa na thamani ya dola 662 za Kimarekani (takribani Tsh 1,487,000/= kwa sasa).
50 Cent hakuzitoa pesa hizo kwa wakati huo na ata akazisahau kabisa, na katika miaka hii michache thamani ya bitcoin imepanda juu sana na ndio amekumbuka kuhusu bitcoin zake. Kwa sasa bitcoin moja inathamani ya dola 11,000 za Marekani (zaidi ya Tsh Milioni 24) na hivyo kwa ujumla wake bitcoin 700 zina thamani ya zaidi ya dola milioni 7 za Marekani.
*Dola milioni 7 za Kimarekani ni zaidi ya Tsh Bilioni 15.7
*Albamu hii ya Animal Ambition ni moja ya albamu yake iliyokuwa imepewa sifa ya kufanya vibaya zaidi kimauzo kwa wakati ule.
Tunauhakika 50 Cent anabonge la tabasamu huko alipo..
Pesa za kidigitali zinapatikana kwa kupitia mfumo wa kielektroniki tuu, hazipatikani kwenye mfumo wa makaratasi kama pesa zingine. Fedha hizi zinatengenezwa kupitia matumizi ya kompyuta – thamani ya nguvu za kompyuta zinazotumika katika kufanya mahesabu mbalimbali makubwa ya data mbalimbali.
One Comment
Comments are closed.