Kampuni ya Mozilla imekubali rasmi ya kwamba mpango wake wa kutoa na kuuza simu zinazotumia programu endeshaji yake ya Firefox OS umeshindwa.
Walishafanikiwa kwa ushirikiano na makampuni kadhaa kutoa simu kadhaa zinazotumia programu endeshaji hiyo lakini hazikufanikiwa sana kimauzo. Soko la programu endeshaji limekuwa gumu sana kutokana na mafanikio makubwa ya programu endeshaji ya Android.
Jana Mozilla wamesema ya kwamba wameacha mara moja kusambaza programu endeshaji ya Firefox OS kwa watengeneza simu. Kwa sasa wanaboresha programu endeshaji hiyo iweze kutumika katika vifaa janja mbalimbali (Internet of Things) nje ya simu. Hii inamaanisha programu endeshaji hiyo inaweza tumika kwenye vifaa kama vile vya nyumbani, viwandani n.k.
Mozilla ni shirika lisilo la kibiashara na linategemea misaada mbalimbali. Kwa kipindi cha miaka kadhaa hivi karibuni kivinjari chao cha Firefox kimekuwa kikipoteza umaarufu na kupoteza watumiaji wengi wanaohamia kwenye kivinjari kutoka Google. – Google Chrome.
Uamuzi wa kuja na programu endeshaji kwa ajili ya simu na tableti ulikuja ili kuleta uwepo wa programu endeshaji ya ziada nje ya Android na iOS. Ata walipopachagua kwa sasa, yaani programu endeshaji ya vifaa mbalimbali tayari kuna ushindani mkubwa, kuna matoleo spesheli ya Android, Windows, WebOS n.k ambayo pia tayari yanatumika katika maeneo hayo.
No Comment! Be the first one.