Kwa mantiki hiyo ni kwamba chini ya 8% ndio zinapigwa na kamera za kawaida? Hii inamaanisha teknolojia ya simu janja imelibadilisha soko zima la kamera kwa kiasi kikubwa sana.
Mpaka kufikia huku kuna mambo kadha wa kadha ambayo yamebadilisha kabisa mfumo, moja wapo ikiwa ni mitandao ya kijamii. Mitandao hii imebadilisha kabisa mfumo mzima wa kupiga picha kwa kutumia kamera za kawaida kubadilika na kuhamia katika simu janja.
Fikiria kipindi kile kabla kabisa ya mitandao hii (FB,IG,Twitter, WhatsApp n.k) tulikua tunategemea kamera za kawaida ili kupata kumbukumbu kwa njia ya picha.
Tulikua tunapiga picha hizo na zinaenda kusafishwa huku nyuma sisi tunaombe situfikie salama –zisiungue—na kisha tunazihifadhi katika vitabu maalum (album).
Baada kuibuka kwa mitandao ya kijamii na simu ambazo zinajikizi ki sawasawa katika swala zima la kupiga picha hali imebadilika kabisa.
Kwa sasa kila mtu anaweza akajipiga picha hata mwenyewe kwa kutumia simu yake, jambo ambalo zamani lisingewezekana mpaka kuwe na mtu zaidi ya mmoja – japo baadae hili lilibadilika.
Utafiti huu umefanywa na Max Spielmann ambao wanasifika kwa kuwa na vituo vingi sana vya kuchapa (print) picha huko ulaya.
Kingine kinachopelekea namba hii kuongezeka ni kwamba mamilioni ya picha yanapikwa kwa kutumia muda mchache sana tofauti na zamani tena kwa kutumia simu janja.
Ukaichana na picha tuu hata kwenye upande wa kurekodi filamu au hata video fupi fupi za kitaalam wengi siku hizi wanatumia simu janja (kuna video nyingi zimeandaliwa kwa kutumia iPhone)
Ubadilishaji wa aina ya kamera umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ujio wa mitandao ya kijamii kwani iko wazi kwamba kuna watu huwa wanatupia picha mara kwa mara katika mitandao yao ya kijamii kwa sababu tuu wana uwezo wa kutumia picha katika simu janja zao.
Ukfikiria ni kwamba mitandao mingi ya kijamii siku hizi haiji kwa lengo la mawasiliano ya moja kwa moja kama ilivyokua zamani.
Mingi inakuja katika mfumo wa mtu ku’share picha au video huku eneo la meseji likiwa lina sehemu yake ambayo haiku wazi wazi kama sehemu ya picha na video.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani matumizi ya kamera za kawaida yatakuja kutoweka kabisa kwa sababu ya simu janja?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.