Pengine tumeizoea kampuni ya Acer katika utengenezaji wa kompyuta na simu janja ambazo kwa muda mrefu sana zimekua zikifanya vizuri sana katika soko. Kwa sasa kampuni inawashangaza wengi maana inakuja na baiskeli janja katika soko.
kumbuka kwa dunia ya sasa ni rahisi sana kwa makampuni haya kuja na bidhaa mbalimbali na kuzifanya kuwa janja zaidi ya vile pengine zilikua mwanzoni.
kingine kikumbukwe ni kwamba sio mara moja kwa kampuni kuja na aina hii ya baiskeli maana hadi sasa kuna makampuni mengi ambayo yana bidhaa hii.
mfumo huu wa baiskeli unakwenda kwa jina la ‘ebike’ lakini Acer wao wameipa jina la ebii na itakua inatumia mfumo mzima wa akili ya bandia yaaani artificial inteligency/AI na hii yote ni katika kuhakikisha kuwa inawasaidia na kuwapunguzia kazi kubwa madereva wa baiskeli hiyo.
ubunifu huo mkubwa na wa aina yake umeifanya kampuni kuinua kifua na kusema moja kwa moja kwamba utawasaidia sana wateja wake kama njia ya usafiri wa hapa na pale.
betri ya baiskeli hii inatembea mpaka maili 68 mpaka kuisha kwake ili kuweza kuchajiwa tena lakini kingine ni kwamba betri hilo linaweza likawa kama ‘power bank’
Yaani kuwa ‘power bank’ kwa vifaa vingine kama vile simu n.k. kumbuka ili betri hilo lijae ni kuchaji kwa masaa mawili na nusu tuu.
Sifa nyingine ya baiskeli Ebii ni kwamba inajibadilisha gia yenyewe na hii itategemea sana na aina ya barabara ambayo baiskeli hii inapita.
Kama baiskeli zingine tuu za aina hii zilivyo ni kwamba hata kama betri ikiisha chaji mtumiaji anaweza akawa anaendesha kwa kutumia njia ya kawaida ya pedeli.
Ningependa kusikia kwako je unaweza ukanunua baiskeli za mfumo huu na kuanza kutumia kama njia yako ya kila siku ya safari zako za hapa na pale, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.