Adobe ni moja kati ya programu kubwa sana za kuhariri picha au kutengeneza kabisa picha kwa muonekano ambao wewe unautaka, ukiachana na maswala ya picha bado kuna vitu vingi inaweza kufanya kama vile kuandaa nembo n.k
Wimbi la AI (Artificial Inteligency) limeingia kwa kasi na kwa sasa kampuni hiyo imeamua na yenyewe ijikite katika teknolojia hiyo. Adobe wanafikiria kuja na firefly.
Adobe wao programu kubwa ambayo waitumia katika maswala mazima ya kuhariri picha ni Photoshop na ilustrator na kwa sasa wana mpango wa kuhakikisha wanakuja na teknolojia ambayo itarahisisha kufanya kazi kwa programu zake hizo.
kitu ambacho teknolojia hii itafanya ni kuhakikisha kuwa inafanya kazi –ambayo umeiamuru– lakini kumbuka tuu kwamba kwa zamani ilibidi kazi hiyo uifanye wewe.
Akili ya bandia ambayo itatumika hapa sio ngeni maana makampuni mengi yanatumia teknolojia ya aina hii kwa tafsiri hiyo ni kwamba kwa kampuni kubwa kama adobe ilibidi iwe imeshakuja na teknolojia hii zamani tuu.
Kwa haraka haraka ni kwamba teknolojia hii ya Firefly itasaidia kwa kiasi kikubwa kusaidia mtumiaji kutumiia akili nyingi na kufanya kazi kubwa mwenyewe wakati teknolojia hii inaweza kumaliza kila kitu.
Mfano unaweza dhahiri ukaiamuru teknolojia hii kufanya kazi fulani kama vile unaweza ukaiamuru iongeze mwanga katika picha na mengine mengi.
mpaka sasa Adobe ina teknolojia nyingi za mfumo wa AI na zinafanya kazi katika baadhi ya App zake lakini kwa ile ya hali hii ndio itakua mpya kabisa, kwa sasa iko katika hatua za mwanzo mwanzo.
Kumbuka teknolojia kama hizi zikiingiaga katika App kama hizi huwa zinawezesha kwa kiasi kikubwa hata wale ambao hawawezi kutumia App hizo wawe na uwezo wa kuamuru tuu teknolojia hiyo iwafanyie kitu fulani
Mpaka sasa haijulikani ni lini teknolojia hii itaanza kutumika rasmi katika App hizo za Adobe lakini kingine kikubwa ni kwamba hatuna budi kusubiri mpaka wao wakatavyotoa taarifa rasmi juu ya lini wanaweka huduma hiyo katika App hizo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je wewe nmi mtumiaji wa Adobe? unadhani teknolojia hii itakuasaidia kwa kiasi gani?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.