Kampuni la Adobe na Stratasys yametangaza rasmi ushirikiano wao ambao utaleta mabadiliko makubwa haswa kwa wataalamu wa ubunifu duniani. Stratasys ni kampuni linalozalisha printa za 3D (3 Dimensions)
Photoshop ni program inayomilikiwa na Adobe ambayo unaweza ukafanya nayo vitu vizuri, vya kuvutia na saa zingine visivyoelezeka — Binafsi, naikubali sana — Pia ni program inayotumika sana duniani katika masuala ya picha kama vile kuzihariri (Edit) N.k
Ushirikiano huu ulitangazwa katika Adobe MAX 2015 iliyofanyika huko Los Angles marekani. Na Kizuri kuhusu ushirikiano huu kwa watumiaji ni kwamba utawahi kuanza. Pia ushirikiano huu umekuaja baada ya mwaka tangia kampuni la adobe lifanye maboresho kwenye Adobe Creative Cloud juu ya swala la 3D. Hii inamaanisha kuwa maboresho hayo yalikuwa kwamba, watumiaji wangeweza kufanya ubunifu wao wa 3D na kisha kuupeleka katika mafaili yenye mfumo wa 3D bila kuwa na shida yeyote.
Ushirikiano huu utajikita sana katika kuhakikisha matumizi ya 3D printing yanafanyika haswa kwa watumiaji wa Adobe CC. Kutokana na hili watumiaji watakuwa na uwezo wa kutuma mafaili yao ya 3D kwa ajili ya kutengenezwa kupitia ‘Stratasys Direct Express’
Pia kampuni ya adobe inatafuta njia ya aina yake katika swala zima la 3D. Tegemeo lake ni kupata njia ambayo itawezesha au italeta uwezekano wa kubeba rangi kama ilivyo katika ubunifu na kuipeleka mpaka katika hatua ya mwisho (ikiwa ime’print’iwa) bila kupoteza uhalisia wowote. Hii yote itakuwa ni muhimu kwa wale wanao ‘print kwa kutumia mfumo huu wa 3D na kwa sasa hata rangi zinakuwa kidogo hazipo katika uhalisia katika mfumo wa ku ‘print’ kwa 3D
Kumbuka kampuni la Adobe na hili la Stratasys wana lengo sawa, Lengo hilo ni kuwapatia watumiaji wake uwezo wa hali ya juu unaohisiana na maswala ya ‘3D printing’ na pia kuwawezesha kutengeneza vitu vya kibunifu ambavyo hakuna mtu aliyeweza fanya.
No Comment! Be the first one.