
Adobe inasheherekea maadhimisho ya miaka 25 ya Adobe photoshop, Software inayoongoza kwa umaarufu duniani inayohusika namasuala ya ku ‘edit’ picha tofauti tofauti. Adobe photoshop imekua na matoleo (updates) mengi sana kiasi cha kwamba unaweza usiwe unajua toleo lake la kwanza.
Toleo la kwanza la Adobe photoshop (Ps) liliachiwa mwaka 1988. Ndio toleo la 1988 linaifanya adobe kuwa na miaka 27 lakini toleo hili halikuachiwa wazi katika jamii. Ilikua ndio toleo la kwanza kujulikana amabalo ni toleo (version) 0.07.
Ps ilipata umaarufu wake baada ya kutoa toleo katika kompyuta za windows mwaka 1992. Hatua nyingine ilipigwa na Ps baada ya kutoa toleo lingine la 5.5, 6.0, 7.0, 7.0.1 ….

Hivi sasa Photoshop ipo katika toleo la 15.0 ambalo linajulikana kama ‘Creative Cloud 2014’ . Photoshop sasa inawaruhusu watumiaji wake kulipa kiasi kidogo kila mwezi kuliko kulipia mamia ya madola mwanzoni mtumiaji anapotumia.
No Comment! Be the first one.