Saa zingine unataka kutoa tangazo kataka mitandao yako ya kijamii, na si kwa njia ya maandishi ya kawaida bali kwa njia ya picha katika mfumo wa ‘graphics’. Adobe kwa kutumia App yao mpya ‘Post’ wanaliwezesha hilo kwani utaweza kutengeneza vipicha picha vya aina yake na kuweza kuvitupia katika mitandao ya kijamii.
Adobe ndio kampuni linaloongoza kuwa na programu maarufu sana duniani katika kutengeneza na kuhariri picha (Adobe Photoshop) kutumia kompyuta hata simu. App hii ya Post hautakuhitaji uwe mtaalamu au mjuaji sana wa mambo ya kucheza na picha picha kwani kila kitu itakufanyia.
App hii imeachiwa Alhamisi na Adobe walitangaza wenyewe kabisa kwa kuandika makala katika mtandao wa http://blog.post.adobe.com
Katika makala hiyo walielezea rasmi kuwa wanatoa toleo la App hiyo kwa simu za iOs kwanza (App sasa inapatikana katika iOs tuu) pengine kadri siku zinavyikwenda watato matoleo ya simu zingine pia
![](https://teknokona.com/wp-content/uploads/2015/12/15298-11491-151217-Adobe_Post-l.jpg)
Kwa kutumia App hii ya Post watumiaji wanaweza tengeneza picha za Graphics kwa mda mchache sana na baada ya hapo wanaweza kuzisambaza katika mitandao yao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram, Twitter na Pinterest cha kushangaza pia unaweza kuzituma kwa njia ya meseji za kawaida (multi media) na kwa kutumia barua pepe (e-mail)
Kila mtu ana kitu cha ku’sharee’ inategemea tuu na mtu anae’share’ nae. Adobe wamesema “Iwe ni tangazo au shughuli maalumu,lakini unaweza ukawa haina muda wala utashi wa kutengeneza Graphics zenye hadhi ya juu ambazo zitafanya tujidai, iruhusu Post ifanye hayo yote kwa ajili yako”
Hii hapa ni video kutoka Adobe ikijaribu kuelezea kuhusu App hiyo
Kwa miaka mingi iliyopita Adobe imekuwa ikiongea na watu, mashirika, wajasiriamali, biashara ndogondogo na wote walitoa sauti moja kuwa wapenzi wa Adobe wanahitaji App ambayo itawawezesha watu kutengeneza graphics za aina yake kwa njia rahisi sana na kuzitupia katika mitandao yao ya kijamii.
Kampuni limetumia uzoefu wake wa miaka 30 katika kuhakikisha inaweka vipengengele vya muhimu katika App hiyo ya Post ambavyo vitamuwezesha mtumaji wa App hiyo kuweza kutengeneza picha nzuri kabla hajaamua azitupie katika mtandao upi wa kijamii.
No Comment! Be the first one.