Kama kile kinachoonekana ni muendelezo wa Airtel Yatosha, Airtel Tanzania imeleta kifurushi cha dakika 25 kupiga simu India kwa gharama ya Tsh 3,000/=.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya, Mkurugenzi mkuu wa Airtel, Bw Sunil Colaso alisema “baada ya uzinduzi wa mafanikio ya huduma yetu ya Airtel Yatosha. Leo tunazindua ofa ya mawasiliano ya gharama nafuu na kuwawezesha wateja wetu kuwasiliana na familia, marafiki na washirika wa kibiashara walioko nje ya mipaka ya nchi.
Kwa kiasi cha chini cha hadi shilingi 3,000 sasa wateja wa Airtel wanaweza kupiga simu India masaa 24 kwa siku 7 za wiki. Ofa hii itampatia mteja dakika 25 za muda wamaongezi kwa muda wa wiki nzima…”
Kwa gharama hii Airtel imekuwa moja ya chaguo la bei rahisi zaidi kupiga simu India, kwani kwa gharama za kawaida katika mitandao mingine kwa dakika 25 itamgharimu mtumiaji zaidi ya Tsh 4000 kwa mtandao wa simu kama Zantel wakati kwa mingine inaweza ikawa hadi zaidi ya Tsh 7000 kuongea kwa dakika hizo (Haya ni makadirio).
Kwa kuongezeka kwa watanzania wanaoishi India kwa sababu mbalimbali kama masomo na zinginezo hakika punguzo hili ni muhimu na litakalo wanufaisha watanzania wengi.
Je wengine watafuata? Muda utatueleza….
No Comment! Be the first one.