Wikiendi iliyopita Airtel wametambulisha huduma mbili kubwa nazo ni kadi ya ‘premier’ kwa wateja wake pamoja na kifaa cha huduma ya WiFI kwa ajili ya manyumbani.
Je hutegemee nini katika huduma hizi? Tupo hapa kujibu swali hilo.
Huduma ya kadi ya Airtel Premier itawapatia wateja wakubwa wa mtandao huo nafasi za punguzo la gharama (discounts) katika maeneo mbalimbali kama maduka na pia itawapatia wateja hao nafasi ya kujivinjari katika maeneo spesheli (lounges) katika viwanja vya ndege mbalimbali duniani (kwa makadirio ni zaidi ya viwanja 700 ulimwenguni kote).
Waziri Dk Mary Nagu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu amesifia hatua hiyo akidai Airtel imefanya jambo zuri katika kusaidia ukuaji wa biashara, na mahusiano ya kibiashara.
Airtel Family WiFi – Huduma ya intaneti ya WiFi kwa ajili ya familia. Maarufu kama mobile WiFi, Airtel wameleta kifaa kidogo ambacho utaweza kuweka laini yako na kujiunga bando ya intaneti na kuweza kuitumia kwa vifaa zaidi ya kimoja. Hii itasaidia kupunguza gharama za huduma ya intaneti majumbani kwa kiasi flani.
Vipi, unafikiri unafikiri huduma gani kati ya hizi ni bomba zaidi kwako? Tueleze
No Comment! Be the first one.