Bharti Airtel, kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza kwa kutoa huduma na shughuli katika nchi 20 katika kusini mwa Asia na Afrika, sasa imekuwa ya nne kwa wingi wa wateja (subscribers) duniani.
Taarifa ilisema mwishoni mwa Juni 2012, Kampuni ilikuwa na zaidi ya wanachama milioni 250 wa simu katika utendaji wake, inayoonesha ukuaji wa asilimia 13 kwa mwaka.
Bharti Airtel ilikuwa ya tano kwa ukubwa katika makumpuni ya simu duniani kufuatia ununuaji wake wa shughuli za Zain Group katika mataifa 15 ya Afrika Juni 2010.
Namba moja inashikiliwa na China Mobile ikiwa na wanachama 683,080,000 ikifuatiwa na Vodafone 386,880,000 na Marekani Movil Group kwa wanachama 251,830,000.
Bharti Airtel ina wanachama 250,040,000 wakati nafasi ya nne inshikiliwa na Telefonica Group ikiwa na wanachama 243,510,000.
No Comment! Be the first one.