Airtel Yatosha ni mfumo wa vifurushi vinavyojumuisha dakika za maongezi, meseji na kifurushi kwa ajili ya huduma ya intaneti kutoka kampuni ya simu ya Airtel. Kusoma makala yetu ya kwanza kuhusu Airtel Yatosha bofya hapa. Bado vifurushi vya Airtel Yatosha tunaweza kuvichukulia ni bora zaidi kwa kuangalia bei na huduma unayopata kulinganisha na vya mitandao mingine (ukilinganisha idadi ya dakika, sms na MB/GB unazopewa).
Vifurushi vya mwezi vilivyopo ni kama ifuatavyo;
Tsh 9,999/= Dak 350 SMS Bila Kikomo pamoja na GB 1 ya intaneti.
Tsh 19,999/= Dak 750 SMS Bila Kikomo pamoja na GB 2 ya intaneti.
Tsh 34,999/= Dak 1500 SMS Bila Kikomo pamoja na GB 3 ya intaneti.
Nadhani uamuzi ni mzuri sana, kwani utawasaidia watu ambao hakika huwa wanajua wanatumia dakika nyingi sana kuongea kwa mwezi. Hivyo kulipia mara moja na kusahau kwa muda mrefu suala la vocha ni jambo zuri.
Kitu ambacho kinaitaji kuboreshwa hapa ni upande wa intaneti, hakika tunaweza sema wamebana. Kwa utumiaji wa simu za ‘smartphones’ wangeanza na GB 2 kwenda angalau GB 2.5 kwa kile cha Tsh 19,999/= na kuacha cha tsh 34,999/= kama kilivyo ingekuwa bonge la ‘deal’. Na dakika zingeanza na 400 hivi 🙂 {nadhani kwa dakika milele haziwezi kutosha}… Ila ni pongezi, ni kitu kizuri kwa wateja wao.
Tusubiri tuone nani atafuata….
No Comment! Be the first one.