Sifanyi kampeni ila shirika la simu la Airtel Tanzania linastahili pongezi kwa kuleta kitu ambacho kilikuwa kinaitajika kwa muda mrefu sana. Tumeona gharama bungufu maarufu kama promosheni, na mifumo mingine mbalimbali ya punguzo la gharama za kupiga simu ambazo zimekuwa zinawalazimisha watu wamiliki laini za simu nyingi ili waweze kunufaika na pungufu hizo. Lakini pungufu moja la kukuruhusu kupiga mitandao yote na kutoa ulazima wa kumiliki laini tatu na zaidi ni kitu ambacho Airtel pekee imekuwa wa kwanza kufanya.
Na zaidi ya yote ni kupitia vifurushi vilivyobuniwa vizuri kuzidi kumpunguzia mteja gharama za kulipia huduma nyingi zaidi.
Huduma hii ya Airtel Yatosha itamuwezesha mtumiaji kulipia gharama moja ya malipo kabla na kupata idadi za dakika za kupigia mitandao yote Tanzania, pia idadi flani ya ujumbe mfupi na bila kusahau kifurushi kukuwezesha kutumia intaneti/mtandao. Vyote ndani ya kapu moja na malipo yanayolingana na uhitaji wako.
Navyo ni kama ifuatavyo;
VIFUSHI VYA SIKU
- Tsh 349 Dk 10 sms 100 MB 25
- Tsh 499 Dk 15 sms 200 MB 75
- Tsh 749 Dk 25 sms 400 MB 150
- Tsh 999 Dk 35 sms 500 MB 250
VIFURUSHI VYA WIKI
- Tsh 1,999 Dk 70 sms 700 MB 175
- Tsh 2,999 Dk 110 sms 1,400 MB 500
- Tsh 4,499 Dk 175 sms 2,800 GB 1
- Tsh 5,999 Dk 250 sms 3,500 GB 1.5
Kujiunga piga *149*99# alafu fuata maelekezo.
Nimejiunga huduma hii kwa majaribio, nimejiunga huduma ya gharama ya Tsh 5,999/=, ya wiki. Nimepigia mitandao ya tigo na vodacom, na kwa kuwa baada ya call unaambiwa umetumia shillingi ngapi basi nimejikuta nikiongea dakika kadhaa baada nakutwa nimekatwa shillingi chache sana, takribani shillingi 3 kwa dakika, sio mbaya.
Kwa upande wa intaneti sishauri kuitegemea sana kwa matumizi makubwa kama kushusha (download) mafaili makubwa kama filamu, kwani nilipo inashika 3G ila mwendo kasi wa intaneti ni kawaida sana kb 15 hadi 38 hivi. Ingawa hii ni ndogo bali kwa matumizi ya kwenye simu na tableti inatosha kabisa, na nadhani hayo ndo matumizi yaliyolengwa. Kwa matumizi makubwa ya intaneti bado naendelea kushauri Vodacom na Zantel.
Ushauri kwa Airtel na Mashirika Mengine: Kwa nini msingeweka na kifungu cha mwezi kabisa? Itakuwa rahisi kulipia tsh 9,999/= au 10,000/= na kusahau suala la kukwangua vocha kwa mwezi. 🙂 !!!!
Niambie wewe unaionaje hii huduma?
No Comment! Be the first one.