Je kuna hatua za usalama za kufuata wakati wa upigaji wa picha za selfi? Upigaji wa picha za selfi ‘unaweza kuwa hatari kwa maisha yako’
Mtu mmoja huko jijini Washington Marekani amefariki Jumapili iliyopita baada ya kujipiga risasi bahati mbali alipokuwa anapiga picha za selfi na silaha akiwa na mpenzi wake.
Mwanaume huyo wa miaka 43 alikuwa akipiga picha za selfi mara kadhaa akiwa na mpenzi wake huku akihusisha bunduki yake kwenye picha hizo.
Inasemekana ingawa alikuwa ametoa risasi katika bunduki hiyo kumbe moja ilisahulika na ndiyo iliyofyatuka wakati akiwa katika upigaji wa picha ya selfi huku akiwa ameelekeza bunduki usoni mwake.
Huyu si mtu wa kwanza kufariki akiwa anajipiga selfi. Kwa miaka ya hivi karibuni watu wengi wamekuwa wakiumia na ata kufa kutokana na kupenda sana kupiga picha za selfi bila kuangalia wakati na mahali wapigapo picha hizo.
Kuna kijana mdogo miezi kadhaa nyuma wa nchini Marekani alijeruhiwa vibaya na kulazwa baada ya bastola aliyokuwa anapiga nayo selfi kumfyatukia na kumjeruhi vibaya na risasi shingoni.
Je una maoni gani juu ya upigaji wa picha za selfi? Je huwa unahakikisha usalama unapopiga picha hizo?
Vyanzo: NYPost na mitandao mbalimbali