Akaunti ya Facebook ya Meya wa Ilala ‘imehackiwa’! Kupitia akaunti yake ya Twitter na Instagram Meya Jerry Silaa adai kuna mtu aliyetumia akaunti hiyo na kutuma ujumbe kwa marafiki zake ‘akidai’ anamaongezi nao ya siri.
Napenda kuwajulisha marafiki zangu wote kwamba akaunti yangu ya facebook ime-hackiwa na kuanza kutuma… http://t.co/U34OoReGOs
— Jerry Sila
a (@JerrySilaa) June 15, 2014
Watu wengine walikuwa wanauliza, ‘hata wewe wanakuhack’… Kwa kifupi ni muhimu sana kuwa mwangalifu na anuani (linki) zozote unazotumiwa kupitia sehemu yako ya ujumbe wa siri Facebook. Uliza anuani hiyo inahusu nini, hii itasaidia kwani kama mtu hakukutumia itakuwa ni rahisi yeye kukujibu na hivyo kugundua kuwa akaunti yake imeathiriwa, kwa kila mwingine anavyobofya ndivyo ujumbe huo unavyoenea kwa wengine na wengine. Kujua zaidi kuhusu suala hili soma makala ‘ JIEPUSHE Na Ku’click ‘Link’ Zisizo Na Maana Kwenye Mitandao Ya Kijamii’ – bofya hapa!
Timu nzima ya Teknokona inampa pole Mheshimiwa Meya, cha kushukuru hakuna cha ajabu kilipostiwa kwenye akaunti yake.
No Comment! Be the first one.