Mwishoni mwa mwezi uliopita Google katika mkutano mkubwa MWC 2018 ilipozindua rasmi mfumo wa Android Go, simu janja ya kwanza kutumia mfumo huo imekuwa Alcatel 1X.
Alcatel 1X nayo imezinduliwa rasmi katika mkutano wa MWC 2018 ikiwa na Android Oreo (Go Edition).
Simu hii ya kiwango cha chini itakuwa na ukubwa wa kioo cha 5.3-inch (960×480 18:9 display).
Pia itatumia Prosesa ya Quad-core MediaTek na ukubwa wa RAM utakuwa ni 1GB na ukubwa wa uhifadhi
ni 16GB.

Kwa upande wa kamera ni kwamba ya nyuma itakuwa na 8MP na ya mbele (Selfie) ina 2MP.
Ujazo wake Betri ni 2,460mAh.
Simu janja hii itaanza kuuzwa mwezi April na matarajio ya bei yake ni kutokuzidi dola 100.
Mbali na Alcatel 1X simu zingine zitakazokuwa na Android Go ni Nokia 1, GM 8 Go, LAVA Z50 na ZTE Tempo Go ambazo nazo zilizinduliwa Kwenye MWC 2018.

