Kutoka na ujio wa kishindo wa Apple Pay na NFC katika iPhone 6 inaonyesha kabisa 2015 utakua ni mwaka ambao malipo kwa kutumia simu (Mobile payments) yataongezeka.
Tayari mamilioni ya watu wanatumia Google Wallet, Paypal na Venmo kulipa bidhaa mbalimbali wanazo nunua katika masoko ya simu/mtandao. Lakini Alibaba anapeleka vitu kwenye sayari nyingine kabisa anapokuja na teknolojia ya “Pay-By-Selfie” yaani lipa kwa kupiga picha ya selfi!
CEO wa Alibaba, Jack Ma, alikua akionyesha teknolojia mabayo inatumia kutambua sura (facial recognition) ili kutumia kupiga picha ya uso maarufu kama selfie ili kununua vitu katika soko hilo. Hivi sasa teknolojia hii inafanyiwa majaribio na ‘Ant Financial’, kitengo cha nje cha Alibaba kinachojihusisha na malipo ya mtandaoni
Ma, aliweka wazi katika mkutano wa CeBit huko mjini Hanover, Ujerumani pale tu alipokuwa anamalizia hutuba yake. Alionyesha watu jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi kwa kumnunulia zawadi meya wa Hanover laivu katika ukumbi.
CEO huyo kwa mbwembwe alibofya kitufe cha “Buy” katika App aliyoiita “Smile to Pay,” na kujipiga selfie kisha akatangaza kuwa zawadi hiyo itawasilishwa kwa meya huyo baada ya siku 6
Ma hakuongea maneno mengi sana na pia siku maalumu ya kuachiwa kwa “Smile to Pay,” bado haijwekwa bayana. Lakini muongeaji wa kike wa kampuni hili aliliambia gazeti la asubuhi la kusini mwa China kuwa kampuni kama kampuni ina msimamo na imejipanga kimkakati kutoa bidhaa (teknolojia) hiyo.
Alibaba tayari ni moja kati ya soko kubwa katika yale yanayolipwa kwa kutumia mtandao (online). AliPay ambayo inafanya kazi kama PayPal tuu ina zaidi ya watu milioni 300 waliojisajili. Wanatoa huduma kwa miamala takribani milioni 80 kwa siku.
No Comment! Be the first one.