Kampuni ya Google kwa muda mrefu ilikuwa inafahamika zaidi kwa biashara zake kupitia teknolojia ya utafutaji mtandaoni yaani ‘Google Search’, huduma ya barua pepe yaani GMail, mtandao wa YouTube na huduma za kimatangazo ya mtandaoni yaani Google Ads.
Lakini hivi karibuni kampuni hiyo imejikita katika mambo mengi zaidi, kama vile teknolojia za magari ya kujiendesha yenyewe, miwani za Google Glass n.k, kutokana na ukuaji huu wameamua kutengeneza kampuni mama mpya waliyoipa jina la ALPHABET na chini ya kampuni mama hii ndio kutakuwa na kampuni zinginezo kubwa zaidi ikiwa ni ya Google.


Kuanzia sana mmoja wa waanzishaji wa kampuni hiyo, Bwana Larry Page atakuwa ndiye bosi mkuu akichukua uongozi wa juu kabisa katika kampuni ya ALPHABET. Chini ya ALPHABET ndio kutakuwa na makampuni mengine tofauti ila kampuni ya Google ikiwa ndio kubwa katika zote.
Kampuni ya Google itakuwa ndiyo inayohusika na biashara na teknolojia za Utafutaji (search), mtangazo (advertising), Gmail, YouTube, na huduma zote zinazohusisha teknolojia ya Android. Google itasimamiwa na Bwana Sundar Pichai ambaye alikuwa ni msaidizi wa Larry wakati Larry akiwa kiongoze mkuu katika Google kabla ya mabadiliko haya.
Bado maamuzi makubwa kama vile bajeti na mishahara ya mabosi wa matawi ya ALPHABET yataamuliwa na kiongozi mkuu wa ALPHABET, yaani Larry
Makampuni mengine chini ya ALPHABET yatakuwa ni Calico (inajihusisha na teknolojia za masuala ya uhai/afya, Google X, Nest Labs, Google Ventures, Side Walk Labs na Google Fiber.
Kwa kuelewa zaidi angalia mchoro huu..
KABLA…

BAADA….

Wengi wanaona uamuzi huu utaweza kusaidia ukuaji wa haraka zaidi kwa kampuni hiyo. Endelea kutembelea mtandao wako wa TeknoKona, mtandao namba moja kwa habari na maujanja ya teknolojia kwa lugha ya kiswahili.
One Comment