Kampuni kubwa zaidi ya uuzaji wa bidhaa mtandaoni ya Amazon kutoka Washington Marekani imehusishwa na taarifa za kutaka kuununua uwanja wa ndege nchini Ujerumani.
Hizi zinaweza kuwa ni jitihada za kampuni hiyo kuboresha huduma zake kwa kushughurikia usafirishaji wa bidhaa zake kwenda kwa wateja. Kampuni hii imekuwa ikipanua wigo wa huduma zake na kwa Marekani kwa mfano imekwisha aanza kufanya jitihada za kukwepa wasafirishaji wa kati.
Tetesi zinasema kwamba Amazon wamefanya mazungumzo na uwanja wa Frankfurt-Hahn ambao umekuwa ukiwapa waendeshaji wake hasara hivyo kuamua kuuza, ingawa haijaeleweka kwamba maongezi ya Amazon na waendeshaji wa uwanja huu yalifanyika lini na yalikuwa juu ya nini lakini kinachojulikana ni kwamba wazabuni watatu(ambao hawajatajwa na pengine Amazoni ni mmoja wao) tayari wamekwisha weka zabuni zao juu ya kununua uwanja huu.
Kwanini Amazon wanunue Uwanja wa ndege?!
Amazon imekuwa ikilaumiwa na wateja wake juu ya ufikishaji wa bidhaa na mara zote wao wamekuwa wakisingizia wasafirishaji ndio wanaochelewesha hivyo kufanya taratibu zote za usafirishaji kutarahisisha huduma za ufikishwaji wa mizigo kwa wateja na hivyo kuwezesha kufikishwa kwa mizigo kwa wakati.
Zaidi uwanja huu upo sehemu nzuri kijiografia, karibu kati ya bara la ulaya ambako kampuni hii imefanya uwekezaji pia na hivyo kuwa na uwanja ambapo ndege kutoka marekani zitaweza kutua kwaajiri ya kuleta mizigo ya ulaya.
Kama kampuni hii itafanikiwa kuununua uwanja huu watakuwa wamepiga hatua na kuweka historia katika biashara za mitandaoni.