Majukwaa makubwa kabisa ambayo yanaonyesha filamu yanayomilikiwa na kampuni ya AMC yako katika makubaliano na kampuni ya Zoom katika kugeuza kumbi zake kuwa uwanja wa mikutano.
Moja kati ya ushirikiano ambao watu hawakuutegemea kabisa ni huu kwa haraka haraka haya ni makampuni mawili ambayo yako (yanfanya mambo) tofauti kabisa.
Baadhi ya majukwaa ambayo ni ya filamu –na vitu vingine vinavyoendana—yatageuzwa kuwa kumbi za mikutano ambayo yanaweza kubeba watu 75 mpaka 150.
Mikutano hiyo itakua ni ile ya mtandaoni (videoconfrence), na kumbi hizo za AMC zitagawa vimiminika na milo laini kama vile bisi n.k yaaani kama vile unaangalia movie
Kingine kuhusiana na hili ni kwamba pengine mkishamiliza mkutano inawezekana hata ukaangalia filamu.
Hapa kinachofanyika ni kwamba makampuni yanaweza yakatuma maombi yao ya kufanya mikutano katika majukwaa hayo katika mtandao—utaratibu upo.
Kingine ni kwamba sio kila jukwaa linalomilikiwa na AMC litakua una uwezo wa kufanya kazi hii ya Zoom, yamechaguliwa majukwaa mpaka 17 tuu kwa sasa.
Hii ni nzuri kwa wafanya kazi ambao hawakai katika eneo moja (ofisi), inakua ni haraka kwao kwenda katika kumbi hizi (zilizo karibu yao) na kuweza kuhudhuria mikutano hii.
Ni wazi kuwa kumbi nyingi za filamu huwa zinafanya kazi usiku (mara nyingi) hii inaweza saidia katika kuhakikisha kuwa AMC inapata hela ya ziada.
Ukaichana na mikutano hii kwa kupitia mtandao wa Zoom bado vyumba hivyo vitatumika katika shughuli zingine za watu kama vile matukio binafsi.
Majukwa haya yatakua yakipatikana katika baadhi ya maeneo huko marekani—pengine yatazidi kuongezeka kama mambo yakiwa mazuri zaidi na watu wakionyesha uhitaji.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hili umelipokeaje? Je unaweza kuhudhuria mikutano ya aina hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.