Bibi Harusi na ubize wa kuchati kwasababisha Bwana Harusi kuvunja ndoa masaa machache baada ya harusi nchini Saudi. Mwanaume alisema sababu kuu ni mke wake kuwa ‘bize’ sana na simu mara tuu walipoingia hotelini, kwenye ‘honeymoon’.
Wadada kueni makini usiku wa ‘honeymoon’ 🙂 weka simu mbali!!!!!
Mwanaume huyo aliezea ya kwamba mke wake huyo mpya alikuwa bize sana na kuchati kuliko kumpa muda yeye. Alielezea ya kwamba mara baada tuu ya kufika hotelini bibi harusi alianza mara moja kutumia simu yake.
Ata bwana harusi alipojitahidi kujisogeza sogeza kimahaba alipatwa na mshituko kuona mke wake huyo akiwa hana’time’ naye kabisa. Alipompiga maswali kuhusu nini kinamfanya awe bize na simu yake mdada alijibu ya kwamba amepata meseji nyingi za pongezi kutoka kwa marafiki na hivyo anazijibu zote kwa wakati huo.
Alipomuomba asitishe zoezi hilo hadi muda mwingine bibi harusi alikataa, hapo Bwana harusi alikasirika na kuuliza kama marafiki ni muhimu sana kuliko yeye…..Bibi Harusi akasema ndio marafiki hao ni muhimu.
Hapo ugomvi ukaanza na Bwana Harusi akatamka kuvunja ndoa hiyo mara moja na kuondoka hotelini usiku huo akimuacha bibi harusi huyo peke yake.
Kwa sasa suala hilo lipo mahakamani ambapo Bwana Harusi ameomba mahakama kuvunja ndoa hiyo kisheria, ndugu waliomba suala hilo litolewe mahakamani ili litatuliwe kwa mazungumzo lakini Bwana Harusi ameshikilia msimamo wa kuvunja ndoa hiyo.
Je wewe unalionaje suala hili? Je jamaa yupo sahihi?
[socialpoll id=”2362464″]
Chanzo: Gulfnews