Google wametambulisha toleo jipya la Android, lenye namba 5.0 linalokwenda kwa jina la Android Lollipop. “‘Lollipop’ kama pipi?” Ndiyo, ni sawa kabisa toleo hili la Android limepewa jina la pipi ya kulamba. Google wamekuwa wakiyapa matoleo yake ya Android majina ya pipi, keki na aiskrimu. Unakumbuka tulipoandika kuhusu toleo hili? Tuliotea jina hili na tulielezea mabadiliko mengi ambayo mengine bado yapo kama tulivyoyataja (Soma- Baada ya KitKat Google Waja na Android L). Kwenye toleo hili la Android Google wajitaidi kufanya mabadiliko mabadiliko kadhaa ambayo ni makubwa sana kimuonekano na kiutendaji. Na hapa nitakuonesha mabadiliko yote makubwa.
NINI KIPYA?
Tegemea muonekano wa kitofauti kwani kupitia Android Lollipop Google wametumia teknolojia yao mpya ya ubunifu wa kimuonekano inayoitwa ‘Material Design’. Wakati Apple kupitia iOS na Microsoft kupitia Windows OS wanaungana na mitandao mingi katika kutumia ubunifu (design) maarufu kwa sasa ya ijulikanayo kama ‘Flat design’, Google wamekuja na kitu kijulikanacho kama ‘Material Design’.
Mabadiliko makubwa katika eneo la taarifa – notifications. Hili eneo moja ambalo wengi wanasema ni zuri kulinganisha na iOS na kwenye Android 5 Lollipop Google wamepafanyia maboresho zaidi. Utaweza kuchagua aina za taarifa za kuwa ‘Priority’, yaani muhimu, na kama basi kutakuwa na ujumbe wowote kutoka kwa watu au apps ulizoziweka kwenye kundi hilo basi ata kamlio ka taarifa kata lia, na kwa baadhi taarifa/notification hii itajitokeza kwa mbele zaidi (pop up). Pia Android Lollipop itaweza kukupatia taarifa kutoka kwa watu unaowasiliana nao zaidi kiutofauti. Hivyo itakuwa kazi yako kujiwekea ata listi ya watu na apps muhimu ambao hutaki kukosa taarifa kutoka kwao.
Recent Apps – Historia ya utumiaji apps nayo imeboreshwa. Kwa sasa inamuonekano bora zaidi, ukibofya kuangalia historia ya apps ulizotumia zitapangwa kimfumo wa kadi na ata kusogea kwake kumewekewa mvuto flani. Tazama picha chini
Mutli-user, yaani uwezo wa kuwa na akaunti tofauti za watumiaji. Hili ni maarufu kwenye kompyuta lakini kupitia Android Lollipop linakuja kwenye simu pia tena likiwa limeboreshwa zaidi kwani kupitia Android 4.2 Kit Kat tayari kwenye tableti za Android kungekuwa na akaunti zaidi ya moja ya watumiaji. Kwenye simu kila akaunti za nyongeza utakazoweka zitakuwa zinajitegemea kidata, mtumiaji hataweza kuona vitu meseji zako, na mambo mengine. Ata vitu kama gemu basi taarifa hazitaingiliana, yeye akicheza atakapoishia na wewe ulipoishia havitachanganywa.
“Okay Google”, zungumza na simu yako ata pale ikiwa imelala (standby/kioo kimezimika), ukiitamkia ‘Okay Google’ itaamka na kuweza kupokea ‘command’ kwa jinsi utakavyotamka nayo….hapa ufahamu lazima kimombo kihusike kwani ukiitamkia kibantu hamtaelewana 🙂
Kuamka kutokana na mguso au msogezo. Simu yako ikiwa imelala basi utaweza kuiamsha kwa kugusa kioo au kuisogeza kidogo na sehemu ya taarifa/notifications inakuja na kukuwezesha kuchungulia kidogo kujua unapitwa na nini. Hii ni tofauti na sasa ambapo kwa simu nyingi ni lazima uminye kidogo sehemu ya kuwashia au ubofye sehemu ya ‘Home’.
Kitu kingine muhimu sana kwa wenye hofu za wizi wa simu ni kuwa kwenye toleo hili kuna kitu wataalamu wanakiita ‘Kill Switch’. Mamlaka za mataifa makubwa kama huko Ulaya na majimbo ya Marekani kama California tayari wanapitisha sheria za kutaka simu zinazouzwa maeneo yao zije na teknolojia kuzuia simu zilizoibiwa kufanya kazi. Kupitia Android Lollipop itakuwa vigumu zaidi kufuta simu (RESET), kwani itakuitaji kuingiza neno/namba siri (PASSWORD/PATTERN) kisha kuingiza barua pepe ya Google akaunti ya simu hiyo pamoja na neno siri lake. Ukifanya hayo yote ndiyo utaweza kufuta simu. Kutokana na hili inategemewa kupunguza wizi mkubwa unaokua hasa kwa simu za Android ukilinganishwa na za iPhone ambazo tayari mtu awazi kufuta bila kuingiza neno siri la Apple ID ya simu husika.
Na pia kama unatumia vifaa vyenye bluetooth nyumbani au kazini au sehemu yeyote unayouhakika na usalama wake unaweza kuchagua simu yako kutojifunga (kuweka LOCK) ukiwa eneo lenye bluetooth ya kifaa flani/husika.
JE UTAIPATA LINI na KWA SIMU ZIPI?
Kwa watumiaji wa simu za Google maarufu kama Nexus wategemee kuweza kupata ‘update’ hii mapema zaidi ikilinganishwa na simu zingine. Kwa sasa simu mpya kutoka Google, ya Nexus 6 ndiyo inakuja na toleo hili. Google wamesema simu zifuatazo zitasapotiwa katika Android Lollipop – Nexus 4, Nexus 5, Nexus 7 (2012), Nexus 7 (2013), na Nexus 10.
Kwa simu kutoka makampuni mengine kama Samsung inategemewa itachukua muda kidogo na kama kawaida toleo ‘official’ kutoka makampuni hayo hawatayatoa kwa simu zote, na inategemewa kwa Samsung toleo hilo litakuja kwa Galaxy S5, Galaxy Note 4, Galaxy Tab S, Galaxy Alpha, Galaxy Note 10.1, Galaxy Note 8.0, Galaxy Note 3, Galaxy Note 3 Neo, Galaxy S5 Mini, Galaxy S5 Active, Galaxy S4, Galaxy S4 Active, Galaxy Tab Pro na Galaxy Note Edge. Motorola, Android 5 itapatikana kwa simu za Moto E, Moto G na Moto X.
No Comment! Be the first one.