Mchoro wa kikatuni cha Android kimenaswa katika mtandao wa Google Maps eneo la nchini Pakstani kikiwa kimechorwa kinakojelea alama ya kampuni shindani ya Apple.
Google Maps ni huduma ya ramani inayowawezesha watumiaji mbalimbali duniani kutambua maeneo kwa urahisi iwe ni kwa kutumia vivinjari vya simu au kompyuta au kwa kutumia app/programu zake za simu, tableti na kompyuta.
Picha hiyo iligunduliwa mapema leo, na Google wamesema si wao walio fanya jambo hilo na dakika chache zilizopita wamefanikiwa kuondoa mchoro huo. Wanadai mchoro huo utakuwa umewekwa na watu au mtu mwingine kwa kutumia mipangalio ya Google Maps inayowawezesha watu mbalimbali kuweza kuonesha na kuandika kuhusu sehemu mpya.
Je unadhani jambo hili linaweza likawa limefanyika na mtu anayeipenda Android sana? Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya Teknolojia!
No Comment! Be the first one.