Unapiga picha halafu huwa hazijiweki kwenye kadi ya ziada? yaani ile SD au wengi wamezoea kuita memori kadi. Kwa wengine inaweza ikawa ni kitu kidogo ila kuna mengi sana katika simu zetu janja siku hizi kiasi ya kwamba inabidi kujifunza vitu vingine vidogo kama hivi.
Kuna faida nyingi za kuhifadhi picha kwenye memori kadi, kwa mfano inakuwa rahisi kuhamisha pale unapobadilisha simu n.k. Kama umekuwa unasumbuka muda mrefu jinsi ya kuwezesha picha ziwe zinaenda moja kwa moja kwenye memori kadi baada ya kupigwa leo utafahamu jinsi ya kuwezesha hilo. 🙂
Njia hii inaweza kutumika katika simu karibia zote za Android zenye uweza wa kuweka kadi ya SD.
Njia ya kwanza;

Hakikisha simu yako ina memori kadi tayari, kisha fungua app yako ya kamera. Kama mara zote picha zilikuwa haziendi kwenye memori kadi basi kuna ujumbe utatokea ukikuuliza kama unataka picha ziwe zinaenda kwenye memori kadi. Kubali, baada ya hapo picha mpya zitakuwa zinaenda kwenye memori kadi.
Kumbuka ata kama ulikuwa na memori kadi tayari ni lazima uichomoe, kisha ichomeke tena kwenye simu, kisha fungua app ya kamera. Lazima taratibu hizi zifuatwe ndio app ya kamera itakuuliza.
Njia ya pili;
Mfano; umefuata taratibu hiyo na bado hujaulizwa chochote? na picha zako haziendi kwenye memori kadi ukipiga. Basi itabidi tutumie njia inayokuitaji wewe kuifahamu vizuri angalau kidogo app yako ya kamera.
i) Fungua app yako ya kamera kisha bofya eneo la Mipangilio, yaani Settings.

ii)Kisha bofya eneo lililoandikwa ‘Storage’, hapa ndio panakupa uchaguzi wa sehemu ya kuhifadhi picha zikipigwa. Ukibofya hapo basi utaona kuna ‘Device’ na ‘Memory Card’, basi chagua ‘Memory Card’.
Je inakuwaje pale ambapo simu yangu inamemori kadi na njia ya kwanza haifanyi kazi, njia ya pili nikienda kwenye ‘Settings’ sioni chaguo la ‘Storage’?
Mara nyingi unaweza pata tatizo hili kama simu yako inatumia toleo la Android 4.4 KitKat, kufanikisha lengo letu itabidi ushushe na kupakua (install) app moja ya kamera iitwayo ‘MX Camera’.
i) Nenda kwenye Google Play au soko lolote la apps unalotumia na shusha ‘MX Camera’
ii) Ukishaweka app hiyo kwenye simu yako itafute na ifungue, kisha nenda kwenye settings za ndani ya app hiyo
iii)Kisha bofya sehemu imeandikwa ‘camera’, kisha bofya ‘Custom save location’, chagua memori kadi.
iv)Baada ya hapo ata ukipiga picha kwa kutumia kamera ya simu picha zitahifadhiwa kwenye memori kadi
No Comment! Be the first one.