Tarehe 13/4/2016 toleo jingine la majaribio la Android lilitolewa na pamoja na mambo mengine Teknokona imegundua kwamba toleo hili litaleta emoji mpya zenye muonekano wa kibinadamu zaidi.
Kwa mujibu wa mtandao wa The Verge pamoja na kulete emoji ambazo zina muonekano wa kibinadamu zaidi Google pia imeleta uwezo wa kuchagua rangi ya ngozi ya emoji unayotaka kuitumia.
Pengine hii ni moja kati ya vitu vilikuwa vinawatesa watumiaji wa Android na vilikuwa vinawafanya wakose raha hasa inapoikuja swala la kutuma ama kupokea emoji kutoka kwa watumiaji wa iOS. Emoji mpya zitawafanya watumiaji wa Android kutumia zaidi emoji kuliko ilivyokuwa mwanzoni, hii ni kwasababu muonekano wa emoji sasa ni raisi kuelewa alichomaanisha alietuima kushinda ilivyokuwa mwanzoni.
Watumiaji wa bidhaa za Apple wamekuwa wakitumia emoji mpya kwa mwaka sasa, muonekano wa emoji hizo umekuwa ni rahisi kuleta maana iliyolengwa tofauti na emoji za android ambazo kiukweli zilikuwa zinachanganya.