Google wameweka hadharani jina kamili la toleo jipya la Android ni Android Marshmallow , jina la toleo hili la android hapo awali lilifichwa kwa sababu za kimauzo na lilijulikana kwa kifupi tu yaani “Android M“. Toleo hili jipya ambalo ni toleo la 6 la Android lilikwishwa fanyiwa utambulisho wa awali mwezi Mei lakini litatoka rasmi baadaye mwaka huu.
Soma Pia -> Fahamu Android M: Toleo jipya la Android Baada ya Lollipop
Android Marshmallow inafuata baada ya mifumo endeshi ya Android iliyotangulia kama Ice cream sandwitch, jelly bean, Kitkat na Lollipop. Kama kawaida jina hili jipya marshmallow nalo limefuata ule utalatibu wa google wa kutoa majina yanayotokana na peremende huku yakienda kwa mtiriliko wa herufi.
Inasemekana pia kuwa google wanashughurikia simu mbili za nexus ambazo ndizo zitatumika kuoneshea mfumo endeshi huu mpya wa Android Marshmallow.Simu hizi mbili moja imetengenezwa na Huawei na nyingine imetengenezwa na LG na zote mbili zitakuwa na uwezo wa kutambua alama za vidole.
Android Marshmallow imebuniwa kuwapa uhuru wa maamuzi zaidi watumiaji kwa upande wa usalama wa vitumizi, pia imebuniwa na kupewa uwezo zaidi wa kuhifadhi betri ya simu kwa kutumia kitumizi cha doze ambapo simu itakuwa kama imelala isipotumika ha hivyo kupunguza matumizi ya betri.
Soma kwa undani kuhusu sifa kuu za toleo hili katika uchambuzi tuliokwisha ufanya -> Fahamu Android M: Toleo jipya la Android Baada ya Lollipop
No Comment! Be the first one.