Uwezo wa kufungua na kutumia apps nyingi kwa wakati mmoja mithili ya kwenye kompyuta unakuja kwenye Android, na unategemewa kuwepo ndani ya toleo lijalo la Android linalofahamika kwa sasa kwa jina la Android N.
Watu wanaotumia toleo hilo la Android lililokwenye matengenezo wameona uwepo wa uwezo huo wiki hii, na waliojaribisha wamesema uwezo huo unafanya kazi vizuri tuu.
Kama uwezo huu utawezeshwa na kutumiwa ipasavyo basi watumiaji wa simu au tableti zenye vioo(display) kubwa watufaika zaidi na uwepo wa teknolojia hii.
Na kwa Google suala hili litafanya tableti zake zipendwe zaidi kwani itarahisisha zaidi utumiaji wa apps nyingi kwa wakati mmoja – jambo ambalo kwa wakati mrefu limeshindikana kwenye tableti za Android na iOS. Ni tableti zinazotumia toleo la Windows kutoka Microsoft ndio zenye uwezo huo.
Endelea kutembelea chanzo chako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia – TeknoKona!
Vyanzo: AndroidPolice na ArsTechnica