Kuna mtafiti mmoja kutoka kampuni ya Microsoft, Mr Zink, siku chache zilizopita alidai amegundua kwa mara ya kwanza kuwa kuna barua pepe za spam zinazotumwa kutoka simu za Android kwa mfumo wa BOTNET.
Mfumo wa Botnet, Bot Herder ataweza Kuongoza
|
BOTNET ni programu zinazotengenezwa kuambukizwa kwenye kompyuta na vifaa vingine vya intaneti/mtandao kama simu na kwa namna moja kuwa kiunganishi kati ya aliyeitengeza na kompyuta yako. Mtu aliyetengeneza programu hiyo ataweza kuchukua usukani wa kompyuta yako kwa kiasi kikubwa kama vile kutuma barua pepe kwa watu mbalimbali kutoka kwenye anuani zako (kwa watumiaji wa programu za barua pepe kwenye kompyuta).
Suala hili limekuwa maarufu pale lilipoihusisha Android, inayotengenezwa chini ya uangalifu wa kampuni ya Google kwa kuwa Android ni jamiii ya Linux na Google siku zote wamekuwa wakisihii kuwa Android inausalama zaidi kulinganisha na wapinzani kama symbian, na Windows Mobile.
Bwana Zink kupitia blogu yake inayopatikana hapa, alisema ila kitu kimoja kinachoonekana ni kuwa barua pepe hizo maarufu kwa jina la spam zinaonesha kutokea kwa watu wanaotumia programu/app kutoka kampuni ya barua pepe ya Yahoo.
Kampuni inayojihusisha na masuala ya ulinzi wa mifumo ya mawasiliano ya simu, Lookout, wamedai inaweza ikawa ni kutokana na tatizo na app ya Yahoo Mail kwani walishagundua kuwa na matatizo na app hiyo na walishaitaarifu kampuni ya Yahoo.
Hadi Sasa Lawama Kuu inaoneshwa Kwa Kampuni ya Yahoo. |
Kwa upande wao kampuni ya Google wameitetea Android na kusema kuwa bado inaulinzi wa uhakika dhidi ya BOTNET na kuwa kilichofanyika ni kuwa watu hawa wanaotuma barua pepe za Spam wamefanya utundu wa kudanganya kuonesha barua pepe hizo zinatokea katika simu za Android wakati si kweli. Google wanadai watu hao wanaweza kufanya hivyo kwa kuwa inakuwa rahisi zaidi kwa barua pepe hizo kupokelewa na kuingina kwenye boksi la barua pepe safi la mtumiwa na kukwepa kuingizwa kwenye boksi la barua pepe chafu. Hivyo watu hawa wanaweza wakawa wanatumia vifaa vingine tuu kama kompyuta za Windows.
Tutawaletea zaidi sakata litakapoishia, kumbuka aliyedai ugunduzi huu ni mfanyakazi wa kampuni ya Microsoft ambayo ni mmoja wa washindani wa kibiashara na kampuni ya Google.
Kwa Habari Zaidi,
Zink’s Blog http://blogs.msdn.com/b/tzink/archive/2012/07/05/10326639.aspx
Lookout’s Blog http://blog.mylookout.com/blog/2012/07/05/our-thoughts-on-the-android-spam-botnet/
No Comment! Be the first one.