Kama una akaunti ya Google ambayo huijaitumia kwa kipindi cha muda mrefu –inaweza iakwa hata ni miaka kadhaa google wameibuka na jambo lao.
Hii ni taarifa mbaya kwa baadhi ya watu na hata wao Google mwezi uliopita wametoa tamko hadharani kwamba wataanza kufuta akaunti ambazo hazijatumika kwa muda mrefu.
Kwa sasa kampuni imeanza kutuma taarifa fupi fupi za kumbukizi ili watumiaji wake wawe wanataari hii, lakini hapa cha kujiuliza vipi kwa yule ambae hatumii kwa muda?
Kumbuka akaunti hiyo inatumika katika kila kitu kinachohusiana na Google mfano Gmail, YouTube n.k
Ili ufungiwe inamaana akaunti yako ya Google inabidi iwe haijatumika katika sehemu yeyote ambayo inahusiana na Google kwa kipindi cha miaka miwili.
Zoezi hili linaanza leo na mpaka kufikia disemba 1 ya mwaka 2023 basi akaunti hizo ambazo hazijatumika kwa zaidi ya kipindi cha miaka miwili.
Cha muhimu kuzingatia ni kwamba kabla ya kufuta akaunti hizo kampuni itatuma barua pepe za taarifa kwamba jambo hilo linafanyika.
Ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa kampuni kufanya jambo hili? Vipi kwa wale watumiaji ambao wanaladhimika kutotumia kwa muda kulingana na changamoto mbali mbali?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.