Tunapenda kuwatahadhalisha wasomaji wetu juu ya mtindo ulioingia siku za karibuni ambapo watu wasio na nia nzuri wanaweza kufanikisha kupokea mawasiliano yote unayoyafanya katika mtandao wa Whatsapp ikiwa ni pamoja na ujumbe picha na hata video.
Mtindo huu ni unatumiwa zaidi na wanaotaka kuwachunguza wenzi (wapenzi) wao pindi wanapohisi kwamba sio waaminifu.
Wahalifu hawa (pengine anaweza kuwa mpenzi/mwenza wako) wanaingia katika whatsapp ya kwenye kompyuta kwa kutumia credentials zako, baada ya hapo wanaendelea kukuchunguza bila wewe kujua mpaka lengo lao linapotimia.
Inawezekanaje kwa mtu kuona meseji picha na video zako bila kushika simu yako!?
Kwa kutumia whatsapp ya kwenye kompyuta mtu anaweza kuingia katika akaunti yako ya whatsapp(Jinsi ya kuingia katika akaunti yako ya whatsapp web fungua HAPA), mfano umeniachia simu yako kwa dakika mbili tu inatosha mimi kuweza kuingia katika akaunti yako ya web (mtandao) katika kompyuta yangu bila ya wewe kupewa taarifa yeyote. hata kama wewe ukaenda na simu yako Marekani mimi nitaendelea kupokea kila kitu kinachoingia na kutoka katika Whatsapp yako.
kwa kifupi ni kwamba muhalifu anahitaji simu yako mara moja tu kuitumia kufungua akaunti yako ya Whatsapp katika kompyuta yake na baada ya hapo ataendelea kupata meseji unazotuma au kutumiwa, picha unazotuma au kutumiwa na video unazotuma na kutumiwa.
Walengwa wa uhalifu huu;
Huu uhalifu unawalenga watu wa aina mbili (2); moja ni watu walio na mahusiano yaani wapenzi, hapa unafanywa na mpenzi wako kwa lengo la kuchunguza kama “unachepuka”. Pili uhalifu huu unaweza kuwalenga watu wakawaida pale unapofanywa na wezi wa kawaida ambao wanataka kujua taarifa zako na nyendo zako.
Sheria ya makosa ya mtandao inasemaje juu ya hili!?
Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 haisemi moja kwa moja juu ya watu wanaotumia kompyuta kuwa spy wenzao bali kipengele cha 15 kinakataza mtu kutumia mfumo wa kompyuta kujifanya mtu mwingine kwa kutumia kompyuta. Pengine hii itakuwa ni moja ya changamoto ya sheria hii mpya kwamba haiwalindi watumiji zidi ya wahalifu wanaolenga kuwachunguza watu bila ruhusa.
Nini cha kufanya kuepuka kufanyiwa uhalifu huu.
- Walau mara mbili kila siku angalia kama kuna kifaa kinapokea meseji zako; nenda settings> Whatsapp Web> kisha bonyeza> Log out from all computers
- Usimwachie mtu yeyote simu yako ikiwa haina lock, maana ni rahisi kuingia katika akaunti yako ya Whatsapp Web.
No Comment! Be the first one.