Kundi hilo la Anonymous limeweka video katika akaunti yao wakitoa ujumbe huo na kuomba wadukuzi wengine duniani kote waungane nao siku hiyo. Mashambulizi yatalenga kuathiri mitandao yote inayohusiana na mgombea Urais huyo.
Kundi la Anonymous tayari lilishawahi tangaza vita ya kimtandao dhidi ya Donald Trump mwezi wa kumi na mbili mwaka jana mara baada ya mgombea urais huo kudai hatazuia waumini wa dini ya kiislam kuingia nchini Marekani.
‘Ndugu Donald Trump, tumekuwa tukikufuatilia kwa muda mrefu, na tunachokiona ni kitu kisichokubalika/kinachoumiza.’ ndivyo walivyoanza katika video yao hiyo. Katika video hiyo wameonesha mambo mbalimbali aliyoyasema Bwana Trump yasiyokubalika kabla ya kuomba wadukuzi wengine duniani kote kuungana nao tarehe moja mwezi wa nne – (Siku ya Wajinga), katika shambulio hilo.
Tovuti zilizolengwa na mashambulizi ni pamoja na TrumpChicago.com, donaldjtrump.com, trump.com, trumphotelcollection.com, donaldtrump2016online.com na citizensfortrump.com. Tovuti binafsi za kibiashara na zile za kisiasa -kampeni.
Lengo kuu la mashambulizi hayo;
- Kufanya tovuti zake zisipatikane
- Kutafuta data zozote binafsi na za kibiashara ambazo Bwana Trump hasingependa zijulikane. Yaani siri zinazoweza athiri harakati za Trump katika kampeni zake za kuutaka urais.
Unaweza tazama video ya Anonymous hapa;
Je unaunga mkono harakati hii? Endelea kutembelea mtandao wa TeknoKona kuendelea kufahamu kama vita yao itafanikiwa au la. 🙂
Vyanzo: Fortune.com na mitandao mbalimbali