Je niwe na app gani kuhariri picha kwa simu kwa urahisi zaidi? Ikiwa unataka kupiga picha zako ziwe nzuri zaidi, unahitaji apps zenye uwezo mzuri wa kuhariri picha kwa urahisi bila kuathiri ubora na ubunifu katika matokeo. Apps hizi zitakusaidia kufanya picha zako zipate muonekano mzuri zaidi, na zingine kufikia kiwango cha juu – yaani utaonekana wewe ni noma sana katika kuhariri picha.
Hizi ni baadhi tuu ambazo tunaamini ata ukiwanazo 3 -4 kati ya hizi tayari utaweza kuwa unahariri picha kwa ubora zaidi na hivyo kuweza kupata matokeo na comments zaidi kutoka kwa watu utakapozishare kwenye mitandao ya kijamii.
-
Canva:
Moja ya app bora kwa kwa ajili kutengeneza matangazo/grafiki kwa ajili ya matumizi ya kwenye mitandao ya kijamii, blogu, na matangazo ya kuchapisha. Ina templeti nyingi za kupendeza, njia za kuhariri zilizo rahisi kutumia, na uwezo wa kutuma kazi yako moja kwa moja kwenda kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii.
Pakua app ya Canva: Google Play store | AppStore (iPhone)
-
Adobe Express:
Hii ni moja kati ya app bora ya uhariri wa picha wa kwa simu za Android. Ina wawezesha wale wanaoanza kujifunza na pia nafasi wale wajuaji zaidi kuwa na uhuru zaidi katika uhariri wa picha.
App hii inakuja pia na huduma zingine mbalimbali kutoka Adobe; kumbuka Adobe ndio wamiliki wa programu mbalimbali za uhariri wa picha na video hadi kiwango cha kibiashara – watengeneza matangazo wakubwa pamoja na watengenezaji filamu. Fahamu zaidi kuhusu programu zingine za Adobe kwa ajili ya matumizi ya kwenye kompyuta hapa – Fahamu Programu zote za Adobe.
Pakua app ya Adobe Express: Google PlayStore | AppStore (iPhone)
-
ScreenMaster:
App hii ni nzuri kwa ajili kufanyia uhariri screenshot – zila picha za kile kinachoonekana kwenye simu yako. Inakuwezesha kukata, kuongeza maandishi, kuweka stika za emoji, na kufanya mabadiliko ya rangi ya screenshot zako.
Pakua app ya ScreenMaster: Google Playstore |Â
-
Snapseed:
App hii inayomilikiwa na kampuni ya Google ni app muhimu kuwa nao wale wanaopenda picha zilizohaririwa kwa muonekano wa kitofauti; hasa zile za selfi, za mazingira na majengo. Ina njia rahisi za kufanya marekebisho ya uso, urembo wa ngozi, na marekebisho ya mwanga na rangi.
Pakua app ya Snapseed: Google Playstore | AppStore (iPhone)
-
PhotoDirector:
Hii ni app nzuri kwa uhariri wa picha ulio wa kitaalamu zaidi.
App hii inakuja na mambo ambayo kwa mgeni wa masuala ya ubora wa uhariri wa picha wa hadhi ya juu anaweza asiyafahamu. Ina uwezo wa kuhariri picha kwa viwango vya juu, kufanya maboresho ya HDR, na uwezo wa kufungua na kutuma faili yaliyo kwenye mfumo wa RAW.
Pakua app ya PhotoDirector: Google Playstore | AppStore (iPhone)
-
Samsung Photo Editor:
Programu bora kwa watumiaji wa Samsung Galaxy. Ina uwezo mkubwa wa kuhariri picha kwa namna mbalimbali – zile rahisi ambazo tayari unazichagua au kama unataka kufanya mabadiliko makubwa ya vitu kama mwanga nk pia utaweza kufanya. Picha uliyoihariri unaweza ituma kwenye app nyingine yeyote baada ya kumaliza kuihariri.
Pakua (kwa watumiaji wa Samsung Galaxy): Galaxy Store
-
Google Photos:
Google Photos ni app iliyo bora na rahisi kwenye uhariri wa picha Programu bora rahisi ya uhariri wa picha wa kwa simu za Android. Nje ya faida ya kukuwezesha kutunza picha zako mtandaoni (backup) bure, app hii inakuja pia na uwezo mzuri wa uhariri wa picha zako. Unaweza kuchagua aina mbalimbali ya uhariri ambao tayari upo – kama vile kwenye Instagram, au unaweza kujichukulia maamuzi kuhariri vitu kama mwanga n.k mwenyewe.
Pia app ya Google Photos inatumia teknolojia ya AI kuhakikisha itakuwa inaendelea kukupa mapendekezo ya uhariri wa picha zako mpya na ata za zamani mara kwa mara.
Pakua app ya Google Photos: Google Playstore | AppStore (iPhone)
-
PicsArt:
Kwa wale wanaotaka kuonesha ubunifu zaidi katika uhariri wa picha basi ni muhimu kuwa na app ya PicsArt. Inaleta kwa pamoja uwezo wa uchoraji, kuunganisha picha, kutengeneza stika, na kuunda GIF.
Pakua app ya PicsArt: Google Playstore | AppStore (iPhone)
-
Adobe Photoshop Camera:
Hii ni app ya upigaji picha kutoka Adobe yenye nia ya kukufanya uisahau kabisa app ya Camera inayokuja na simu yako. App inakuja na teknolojia ya AI na hivyo inauwezo wa kutambua ni kitu cha namna gani unakipiga picha na hivyo kukupatia mapendekezo ya kimuonekano kabla ya wewe kupiga picha.
Moja kwa moja kwenye eneo la kupiga picha unaweza kuchagua themes za aina mbalimbali ambazo tayari zipo hapo hapo, na hivyo kukupa nafasi ya kuchagua uhariri wa picha kabla ata haujaipiga. Utaweza kuona muonekano utakavyokuwa kabla haujapiga.
Pakua app ya Photoshop Camera: Google Playstore | AppStore (iPhone)
-
Pixlr:
Pixlr ni app inayorahisisha zaidi zoezi la kuhariri picha. Inamuonekano ulio rahisi kwa mtu yeyote kutumia na pia inakuja na ‘effects’ nyingi za kupendezesha picha.
Toleo la bure linakuja na matangazo, ili kuyaondoa inabidi ulipie.
Pakua app ya Pixlr: Google Playstore | AppStore (iPhone)
No Comment! Be the first one.