Kama ulikuwa una mpango wa kujichora tatuu na hujui uanzie wapi App hii inaweza ikawa msaada mkubwa sana kwako. App hii itakuwezesha kupa mitazamo mbali mbali wa jinsi ya tattoo yako mpya jinsi itakavyo kuwa
Ndio, najua kuna wale wanaotaka kujichora lakini hawajui wajichore nini na wale ambao wanataka kujichora ila wanataka wapate uhakika kama hicho kitu kitawapendeza wakijichora au la
App hii inaweza ikajibu maswali yote hayo. App hiyo inaitwa Ink Hunter ambayo inakuletea aina nyingi za tattoo ambazo huenda zikakupendeza pindi ambapo ukiwa umezichora katika mwili wako

Ni rahisi sana kutumia App hii, cha kufanya ni kuishusha na kuipakua. Baada ya hapo unaweza ukaifungua na kuanza kuitumia
Katika kuitumia itakubidi uchore kialama cha tabasamu katika eneo ambalo una mpango wa kuchora tattoo (ukifanya hivi App inaweza kutambua vipimo vya eneo hili) na kisha bofya katika eneo la ‘Tap to add your design’.

Kizuri ni kwamba unaweza hata ukaihifadhi picha hiyo ya tattoo kwenye simu yako na baadae ukiamua unaweza ukaamua kuituma kwa marafiki zako ili wakupe ushauri juu ya tattoo hio.
Kitu ambacho sio kizuri katika App hii (Ink Hunter) ni kwamba michoro yote inaweza ikaonekana katika rangi nyeusi ukiachana na rangi zingine. Kumbuka kuna wengine wanapendelea tattoo zenye rangi kama vile nyekundu.
Lakini kwa kiasi kikubwa rangi ya Tattoo inategemeana sana na rangi ya ngozi ya mtu. Ukiachana na swala la rangi, App hii ilitengenezwa na Oleksandra Rohachova na wenzake walipokutana katika tukio walilliandaa la mambo ya teknolojia.

Ink Hunter imetengenezwa julai 2014, lakini mpaka sasa umeshushwa mara 200,000. App hii imeshushwa kwa kiasi kikubwa mwaka jana na hilo tuu linaonyesha dhahiri kuwa App hii inapanda chati
Kama ni mtumiajia wa iOS pakua App hii hapa na kama wewe ni mtumiaji wa Androi usipaniki, tulia toleo lako liko njiani linakuja.