Kama unasafiri mara kwa mara kwenda nje ya nchi basi App hizi zitakusadia kwa kiasi kikubwa sana. App hizi lengo lake kubwa ni kukupa msaada mkubwa kuanzia pale unapopanda ndege mpaka pale unapofika sehemu uliyokusudia
App hizi pia itakusaidia mambo mbali mbali kama vile hoteli gani ya kufikia, wapi pa kupata chakula au kahawa, kupata ramani ya mitaa Fulani n.k
Kumbuka mara nyingi tukisafiri kwenda nchi za nje tunakuwa ni wageni, na kama tunakuwa ni wageni inamaanisha kuwa kuna baadhi ya mambo tunakuwa hatuyajia kwa kutumia App hizi tunaweza tukajitoa matongo tongo.
Tuzijue App Hizo
1. Google Maps
Katika App za muhimu kabisa za kuwa nazo ni Google Maps. Uzuri wa App hii ni kwamba hata kama umepotea mahali bado unawezo mkubwa wa kufika ulipokuwa unatakiwa kufika kwa msaada wa App hii. Pia App hii ya bure kabisa inaweza ikakupatia njia bora zaidi kati ya nyingi ambazo inabidi uzipitie katika kufika mahali Fulani. Njia hizo zitategemea kama utatembea kwa mguu, kwa basi au hata gari binafsi
2. TripAdvisor
Kama mtandao wake ulivyo tuu App hii inakufumbua macho juu ya mahali Fulani. Yaani itakuambia ni nini wasafiri wengine wanasema kuhusiana na sehemu Fulani ambayo unataka kuitembelea. Kwa mfano unaweza taka tembelea mahali Fulani lakini ukaingalia katika App hiyo unaona kuwa watu wengi waliofika katika eneo hilo hawakufurahia au walipata huduma mbaya basi unaweza ukaamua kwenda sehemu nyingine sio?
3. Zomato
Ukiwa unaenda sehemu yeyote kitu ambacho ni lazima ufanye ni Kula, ndio lazima utakula tuu! Sasa basi App ya Zomato kazi yake kubwa ni kukuonyesha sehemu gani ya mji inasifika kwa kuwa na chakula kizuri. App hii itakusaidia kugundua migahawa mizuri katika eneo Fulani na pia hata kutafuta migahawa ambayo iko karibu yako. Kingine kizuri ni kwamba unaweza soma tathmini ya eneo husika kabla hujaamua kwenda kupata chakula hapo
4. Xe Currency
Kama wewe ni msafiri mzuri wan je ya nchi na huwa unatumia kadi yako ya ATM basi ni vyema kujua kiwango cha pesa ya kigeni kina thamani gani kulinganisha na kile cha nchini mwako kwa siku hiyo. Baada ya kujua hayo itakufanya hata uweze kufanya manunuzi kwa amani kabisa bila kuwa na wasiwasi wowote
5. Google Translate
Tukiwa tunaenda katika nchi za watu kuna hati hati tusiweze kuzungumza lugha zao vizuri au hata kukwama na kushindwa elewa baadhi ya maneno, hapo ndipo Google Translate inapokuja.
Google Translate ni huduma mahususi kutoka Google ambayo inamsaidia mtumiaji kuweza kupata tafsiri ya maneno ya kigeni kwake. Pia ukiwa na unatumia huduma hiyo unauwezo wa kutafsiri mazungumzo kabisa licha ya neno moja moja.