Ni utamaduni wa majukwaa mengi kuweka takwimu za App au hata magemu yao ambayo yamefanya vizfuri katika majukwa hayo, kwa sasa ni zamu ya App Store.
Kuna kipindi tuliandika kuhusiana na Microsoft Store Awards ambapo tuliwaandika washindi wote katika jukwaa hilo pia. Apple kupitia soko lake maarufu la App Store na wenyewe wanakuja na orodha yao ya magemu na App zilizofanya vizuri zaidi.
Tunaangazie kwa upande wa App Store kutoka Apple ni nani kaibuka kinara katika upande wa App na gemu, katika iPhone na iPad n.k
Apps Bora Kwa Mwaka.
App Ya Mwaka Kwa iPhone: BeReal, Kutoka katika kampuni ya BeReal.
App Ya Mwaka Kwa iPad: GoodNotes 5, kutoka katika kampuni ya Time Base Technology Limited.
App Ya Mwaka Kwa Mac: MacFamilyTree 10, Kutoka katika kampuni ya Synium Software GmbH.
App Ya Mwaka Kwa Apple TV: ViX, Kutoka Katika kampuni ya TelevisaUnivision Interactive, Inc.
App Ya Mwaka Kwa Apple Watch: Gentler Streak, kutoka katika kampuni ya Gentler Stories LLC.
Magemu Bora Kwa Mwaka.
Gemu La Mwaka Kwa iPhone: Apex Legends Mobile, kutoka katika kampuni ya Electronic Arts.
Gemu La Mwaka Kwa iPad: Moncage, kutoka katika kampuni ya X.D. Network Inc.
Gemu La Mwaka Kwa Mac: Inscryption, kutoka katika kampuni ya Devolver.
Gemu La Mwaka Kwa Apple TV: El Hijo, kutoka katika kampuni ya HandyGames.
Gemu La Mwaka Kwa Apple Arcade: Wylde Flowers, kutoka katika kampuni ya Studio Drydock Pty Ltd.
Gemu La Mwaka nchini China: League of Legends Esports Manager, kutoka katika kampuni ya Shenzhen Tencent Tianyou Technology Ltd.
CHANZO: 9to5Mac
Je ni nani mwingine katika majukwaa haya atakuaja na orodha yake ya App bora au hata magemu bora kwa mwaka huu? hatuna budi kusubiria sio?
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je unadhani ni sawa kwa App na magemu haya kuwa bora kuliko zingine kwa mwaka huu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.