Muonekano mpya wa app ya Instagram ulio njiani kuanza kusambaa kwa watumiaji wa app hiyo waanza kupatikana kwa baadhi ya watumiaji wa app hiyo.
Kwa muda mrefu app ya Instagram haijafanyiwa mabadiliko yeyote makubwa ya kimuonekano tokea ujio wake na sasa inaonekana mabadiliko yanakuja.
Angalia picha zinazoonesha muonekana huo mpya uliombioni kupatikana kwa watu wote… Je unadhani kuna umuhimu wowote wa kubadilisha muonekano huo?
Muonekano huu tayari umesukumwa kwenye updates za watu wachache huku wenyewe Instagram wakisoma maoni ya wale wanaopata app hiyo katika muonekano huu. Inasemekana kama utafurahiwa na watumiaji wengi basi muda si mrefu utapatikana kwa wote.
Ingawa ni muonekano mzuri ila kwa kiasi kikubwa unaleta mabadiliko makubwa sana ya kimuonekano kwa watu ambao wametumia app hiyo kwa kipindi kirefu.
Unamaoni gani juu ya mabadiliko haya?
Picha na mtandao wa PhoneDog