Je umesikia kwa muda mrefu kuhusu app ya m-paper inayokuwezesha kununua na kusoma magazeti ya Tanzania kwa urahisi kwenye simu yako ila umeshindwa kutumia kwa kuwa hautumii Android?
Sasa fahamu rasmi ya kwamba app ya m-paper imeanza kupatikana rasmi kwa watumiaji wa iPhone na iPad.
App ya m-paper inakupa faida kadhaa kama vile;
- Kubakia na nakala za magazeti yote unayoyanunua ili uweze kuyasoma tena muda wowote
- Pia unanunua kwa bei nafuu zaidi
- Ata unapokuwa mbali na eneo liuzalo magazeti bado hautapitwa na chochote
Unaweza ipata app hiyo rasmi kupitia soko la apps la iOS. -> App Store | Watumiaji wa Android -> Google Play