Apple inarahisisha kuhamisha vitu vya muhimu kutoka katika simu yako ya Android kwenda katika ile ya iOs. Hebu fikiria, umejipatia simu mpya ya iPhone na una baadhi ya taarifa zako za muhimu katika simu yako ya Android ambazo inabidi uziweke katika simu hiyo mpya (iPhone).
Hutatoa jasho tena kama zamani, sasa kila kitu Apple wanakurahisishia. Ukitumia App hii meseji, picha, video, Taarifa za kivinjari (Bookmarks), akaunti za barua pepe, kalenda pamoja na wallpaper vyote vitahamia katika kifaaa cha iOs (iPhone na iPad). Na Cha kuongezea ni kwamba kama kuna App yeyote ya kulipia katika simu ya Android zoezi hili likifanyika App hizo zitawekwa katika kundi la ‘Wish List’ katika kifaa cha iOs (iPad na iPhone)
Zoezi Hili litakamilika kama kifaa chako cha iOs ni kipya au umeki ‘Reset’ tuu. Hii inamaanisha kwa vifaa vya iOs vile vilivyotumika kwa mfano kama umetumia iPhone yako na kisha ukasema unataka uhamishe taarifa zako kutoka simu ya Android itashidikana (Labda ui ‘Reset’ Hiyo iPhone Kwanza)
Tuangalie Habari Picha Jinsi Ya Kufanya Zoezi Hili
- Kwanza kabisa shusha App Ya ‘Move To iOs‘ katika simu yako ya Android.
Zoezi zima la kufanya yote haya ni rahisi na kila mtu nna imani anaweza fanya mwenyewe. Japokuwa App hii katika Google Play store imepata mapokezi hasi (si mazuri) kwa watu wengi na wengi wao wakiwa ni watumiaji wa Andriod. Licha ya mapokezi hayo App hii bado ina msaada mkubwa kwa wale wanaotaka kubadilisha mazingiza (kutoa Android mpaka iOs)
Move to iOS [Android]
No Comment! Be the first one.