Katika nchi ambayo huruhusiwi kuendesha gari, utafika vipi au utazururaje mjini?. Hii ni kwa wanawake wa saudi arabia, Nchi ambayo ina sera maalamu isiyoruhusu wanawake kuendesha magari. Kwa wanawake wengi wa Saudi Arabia App ya Uber ndio kimbilio lao.
Ukiachana na mapendekezo yaliyotolewa na Baraza linalojulikana kama Shura, Kamati ya ushauri ya saudi (Ambayo ki ukweli inakuja na vizuizi vya aina yake). Wanawake bado wanakatazwa kuendesha katika nchi hiyo tena wanakatazwa ikiwa inaogopeka wanaweza kuvunja sheria kama vile kuvua jilbaab,hijab au hata sheria nyingine ya kidini inayohusika na kufunika uso kwa mwanamke ambayo inamfanya awe anaelekeza vizuri macho yake kwenye barabara.
Ingawa hakuna sheria ya kawaida (General Law) ambayo inamkataza mwanamke kuendesha gari. Lakini pia leseni si ndio kila kitu, yaani ndio itakayo kuruhusu kuendesha gari? Cha kushangaza ni kwamba Saudi Arabia hawatoi leseni za udereva kwa wanawake. Ikitokea amekamatwa anaendesha gari adhabu na sheria kali zitachukuliwa.
Kutokana na adhaa hiyo, wanawake wengi wanalazimika kutumia huduma za magari kama vile Taxi kufika katika miji mikubwa kama vile Riyadh, Dammam, na Jeddah.
Ingiwa wanawake wa saudi wanachangia asilimia 13 tuu kama nguvu kazi katika nchi hiyo (Saudi Arabia). Inasemekana (Haina usahihi kwa asilimia 100) kuwa asilimia yoyote kati ya 70 na 90 watumiaji wa Uber nchini saudi arabia ni wanawake. Kama inavyojulikana Uber ni App ambayo inatumika kwa madereva kuwaonyesha ruti tofaui tofauti katika sehemu husika.
Nchini Saudi Arabia asilimia 60 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni jinsia ya kike kulingana na takwimu zilizilizotolewa na Fast Company, zinaonyesha kuwa wanawake hasa kwa sasa wanatakiwa watoke na wazurure na sio zile sehemu ambayo inawabidi wawe tuu bali hati zile wanazohitaji kuwepo
App Ya Uber Ilianza Patikana Kwa Wananchi Wa Saudi Arabia May 2014. Tokea hapo imekuwa ni msaada mkubwa kwa wanawake ambao sera ya kutoendesha gari inawabana
Katika mahojinao yaliyofanyika baina ya Fast Company na Meneja mkuu wa Uber bw. Majed Abukhater alieleza kwa kina juu ya tofauti zipi aliziona tangia App ya Uber inaze kufanya kazi nchini Saudi Arabia na mabadiliko hayo haswa yamefanywa na wanawake.
”Muda mwingine makampuni ya usafiri yalikuwa yanakata tiketi kwa wananchi wa nchi hiyo na kujaza viombo vyao vya usafiri lakini wananchi wengine wakikosa usafiri kutokana na makampuni hayo kusaza. Wanamke kwa upande mmoja au mwingine wangepata shida kuenda sehemu fulani za jijini hapo” alisema Abukhater ”Kwa kuwa tumeongeza teknolojia hii nchini humu sasa mwanamke hatahitaji kupigia simu kwa makampuni 10 au 20 ili kujaribu kupata dereva, wanaweza tuu wakafungua App. Hivyo ndio maana tumeona ongezeko kubwa (ukuaji) mpaka sasa”
No Comment! Be the first one.