Ni wazi kuwa WhatsApp kwa sasa wanataka kupatikana katika vifaa vingi zaidi na kwa sasa wanavifikia vifaa vinavyotumia MacOS.
Kwa sasa toleo ambalo linapatikana ni la majaribio, kama una kumbukumbu nzuri ni kwamba hapo awali mtu alikuwa anaweza kutumia WhatsApp Web katika kompyuta tuu.
Pata picha kwa sasa kuna App spesheli ambayo mtumiaji anaweza ishusha na kuanza kufurahia huduma hii ya mtandao wa kijamii katika kifaa chake ambacho kinatumia programu endeshi ya MacOs kutoka Apple.
Kwa haraka haraka ni kwamba App hiyo haitakua na utofauti mkubwa sana ukilinganisha na ile ya mtandaoni (WhatsApp Web) kwani vipengele vingi sana viko sawa.
Na hata baadhi ya taratibu kama vili ku’scan QR Code kwa njia ya simu yenye WhatsApp bado itakua inafanyika kama vile ilivyokua katika ile ya mtandao (web).
Mpaka sasa mtu anaweza kwenda katika mtandao wa WhatsApp na akashusha App hiyo ambayo kwa sasa iko katika mfumo wa majaribio.
Faili la App hiyo liko katika mfumo wa DMG ambayo ni aina ya fomati ya kusambaza mafaili na App mbalimbali katika vifaa vya Apple sana sana kompyuta.
Hii sio mara ya kwanza kwa mtandao huu wa kijamii kuja na App kabisa kwa ajili ya kompyuta, tuliona mara ya kwanza walianza na windows. Soma zaidi >>HAPA<<
CHANZO: WaBetaInfo
Ni wazi kuwa mtandao huu unajitahidi sana katika kuhakikisha unazidi kuiboresha kwa kuwapa watumiaji wake kile wanachotaka na pia kuiimarisha sana kwa washindani wao wengine katika nyanja ya mitandao ya kijamii
Soma kila kitu kuhusiana na WhatsApp >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, umeshawahi kutumia WhatsApp Web? na je unadhani App hii itapata watumiaji wengi katika MacOS kuzidi ile ya Windows? Je hii umeipokeaje hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.