Zoom ni kampuni kubwa ambayo inajihusisha na huduma ya mikutano ya kimtandao kwa njia ya video.
Kumbuka mtandao wa Zoom ulijipatia umaarufu mkubwa sana baada ya janga la CORONA kutawala dunia tangia 2019.

Kwa sasa inasema App yake katika laptop za Chromebook itaacha kufanya kazi katika laptop hizo ikifika agosti 2022.
Kingine cha kukumbuka ni kwamba janga la CORONA pia liliongeza uhitaji wa laptop ambazo zilikua ndogo ndogo na nyepesi, hapa hata mauzo ya Chromebook yalipanda maana watu walikua na uhitaji mwingi wa laptop hizi.
Unaweza ukawa unajiuliza sasa kwanini mtandao huo unafuta App yake katika Chromebook?

Repoti zilizopo zinasema kuwa App hiyo (Zoom) ipo kwa miaka kadhaa, utumizi wake sio mpana sana na pia tokea muda huo App haijaweza kupata sasisho (update) la maana na lenye tija.
Kikubwa ambacho kinafanya App hii kufutwa moja wapo ni kwamba App hii inasemekana ina hati hati kubwa ya kushidwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa sababu ya toleo linalotumika katika Chromebook ni la zamani.

Kwa mwaka 2020 kama unakumbuka vizuri kampuni ya Google ilisema kubwa itafuta App nyingi sana katika Chromebook na kuwaomba waandaji wa App kuja na App za web kama vile WhatsApp web.
Niandikie hapo chini katika eneo la comment je unafikiri ni wazo sahihi kwa kampuni hii kuweza kusitisha App hiyo au ilibidi kufnaya marekebisho tuu? Ningependa kusika kutoka kwako.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.