Kwa mara ya kwanza kabisa App hizi zinaanza kupatikana kama App katika Windows na zimekua zikisubiriwa kwa hamu sana ndani ya vifaa vya Windows.
Japokua kwa sasa lipo toleo la App hizi ambalo ni kwamba linapatikana katika Windows 11 tuu kwa sasa yaaani hata katika Windows 10 huwezi kulipata

Kama kawaida linapatikana kwa kulishusha kupitia katika soko maarufu la Microsoft yaani Microsoft Store ni ni matoleo ya bure kabisa.
Kama una kumbukumbu vizuri ni kwamba mwaka 2019 Apple ndio waliamua kuigawa iTunes na kuwa katika App mbili zinazojitegemea ambazo ni Apple Music, Apple Tv. Na Podcast.. Soma zaidi >>HAPA<<
Licha ya jambo hili kufanyika kwa wakati huo lakini bado apple walikua ni wagumu kuziweka App hizi kuanza kupatikana katika masoko mengine ya Apple isipokua katika App Store tuu.

Kitu ambacho Apple ilifanya ni kwamba iliacha toleo lile lile la iTunes (kabla ya kuvunjwa kua App mbili) kuendelea kupatikana katika kompyuta za Windows ambapo watu walikua na uwezo wa kupata Apple Music ndani ya App hiyo. Soma zaidi >>HAPA<<
Kingine cha kushangaza ni kwamba kwa watumiaji wa Windows walikua wanaweza kupata Apple Tv+ kwa kuingia kupitia mtandao (kivinjari) tuu.
Kuleta App hizo katika Windows inaleta uwepesi kabisa katika kutumia App za Apple katika Windows na kwa sasa App hizo katika Windows 11 zinaweza zikawa hazifanyi kazi kama zinavyotakiwa.

Hii ni sababu kuwa App hizo ziko katika hatua za mwanzo mwanzo kabisa na Apple wamefanya hivyo kusudi kabisa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je hii umeipokeaje? Na je uko tayari kufurahia app hizo katika Windows 11?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.