Android imebadilisha na kuboresha mambo mengi katika simu zete. Licha ya kuwa programu endeshaji inayotumika sana duniani katika simu zetu kwa sasa, bado kuna mambo kibao tunaweza kufanya kupitia Android. Kaa name kujua njia mbali mbali ambazo utaweza kushusha mafaili ya torrent kupitia Android.
Tumeshaona mambo mengi ambayo kompyuta zetu zinaweza kutufanyia sio? Ukiniuliza kwa sasa ntakuambia wana teknolojia kwa kiasi kikubwa wanatak akuigeuza simu janja kuwa ndio kompyuta yako.
Kuna kipindi ilikua ukitaka kushusha mafaili ya torrent ilikuwa ni lazima utumie kompyuta yako. Leo TeknoKona inakuletea App kibao ambazo unaweza ukazitumia katika kifaa chako kushusha mafaili ya Android. Hebu fikiria unaweza ukashusha filamu nzima kwa kutumia simu yako tuu
App zifuatazo ndizo zinaweza zikakuwezesha kushusha mafaili ya torrent katika kifaa chako
1. tTorrent:
Hii ni moja kati ya App bora kabisa ambazo zinaweza kukuwezesha kushusha mafaili ya Torrent katika kifaa chako cha Android. App hii inatoa huduma nyingi kama vile kushusha faili zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Toleo la App hii la bure linawezesha mtu kushusha faili kwa spidi ya 250 kbps. Kama utataka kushusha mafaili kwa spidi kubwa basi huna budi kupakaua toleo la kulipia la App hiyo
App imepata Sifa Ya Nyota: 4.5 kati ya 5
Shusha Hapa Kupitia Google Play: Bofya Hapa
2. uTorrent (toleo la simu)
kitu kizuri kutoka uTorrent ambacho hakipo katika tTorrent ni kwamba hapa hautapata tabu katika spidi. Yaani hakuna kikomo cha spidi, spidi itategemeana na intaneti yako katika kushusha mafaili.
Unaweza ukashusha mafaili mengi sana ya torrent kwa kupita App hii katika spidi nzuri tuu. App hii ina huduma kama vile za kutafuta (search) na pia utumiaji wa WiFi.
App imepata Sifa Ya Nyota: 4.3 kati ya 5
Shusha Hapa Kupitia Google Play: Bofya Hapa
3. BitTorrent (Kwa Ajili Ya Simu)
Licha ya kuwa Programu moja maarufu sana ya kushusha mafaili ya torrent katika kompyuta, bado imepiga hatua na kuwa katika simu janja pia. Watumiaji wa simu na vifaa vingine vya Android wanaweza wakatumia App hii katika kushusha mafaili ya torrent.
App imepata Sifa Ya Nyota: 4.2 kati ya 5
Shusha Hapa Kupitia Google Play: Bofya Hapa
4. Torrentex
Hii pia ni App ambayo inamuwezesha mtumiaji wa Android kuweza kushusha mafaili ya Torrent kwa urahisi kabisa. Hii inatoa huduma kwa wana Android na pia mafaili yanawezwa shushwa katika spidi kubwa tuu. Vipengele vilivyopo ni kama kile kinachojulikana sana kwa watu wa wapenzi wa mafaili ya torrent kinachojulikana kama ‘magnetic link’
App imepata Sifa Ya Nyota: 4.4 kati ya 5
Shusha Hapa Kupitia Google Play: Bofya Hapa
5. aTorrent
TeknoKona inakuletea hii kama ya mwisho kwa leo – hatutaishia hapa lakini – aTorrent na yenyewe inakupa uwezo wewe mtumiaji wa Android. Inatoa huduma kibao kama vile uwezo wa kutafuta (search), ‘magnetic link’, uwezo wa WiFi, kusimamisha kwa muda na kendelezea mafaili ambayo yanashuka. Katika toleo hii unaweza ukaona matangazo mbali mbali kutoka kwa watangazaji mbalimbali
App imepata Sifa Ya Nyota: 4.4 kati ya 5
Shusha Hapa Kupitia Google Play: Bofya Hapa
Kwa leo TeknoKona imekuandalia hayo kwa leo, maujanja mengi zaidi utazidi kuyapata kuwa na subira tuu