Ni wazi kwamba Apple wana ubinafsi sana hasa katika huduma zao, huduma zao mara nyingi huwa zinaingiliana kwa vifaa vyao tuu na mwanzoni Apple Tv ilikua ni hivyo hivyo.
Apple Tv ni moja kati ya huduma kubwa sana kutoka Apple ambayo inahusisha Ku’Stream kwa malipo ya vifurushi vya awamu ili kuweza kuangalia filamu, michezo ya kuigiza n.k
Kumbuka huduma kama hii inahitaji kwenda mbali zaidi (kuonekana kwa watu wengi) ili kujihakikishia kukua kwa mapato, nadhani hii ni moja kati ya sababu ambazo zinawafanya Apple kutaka kuwafikia watu wengi zaidi.
Mpaka sasa huduma hii inapatikana kwa baadhi ya wadau ambao wanatumia Chromecast zinazotumia Google TV kutoka Google lakini vipi kuhusiana na watumiaji wa Android?
Apple wameweka wazi kwamba wana mpango wa kuleta App ya Apple Tv kuanza kupatikana katika vifaa vyote vya Android.
Hii inamaanisha kuwa App hiyo itaanza kupatikana katika soko la google Play Store ambalo ni moja kati ya masoko makubwa kabisa ya App.
Tayari Apple imeanza kuiweka app ya Apple TV katika baadhi ya Chomecast ambazo zinatumia Google TV. Soon watumiaji wa Android watakuwa na app yake.
Apple TV iko katika vifaa vingi sana kama vile PS4, PS5, Xbox, Roku, na Amazon Fire TV na hata katika baadhi ya TV janja kama vile Sony, LG na Samsung.
Hii inaonyesha dhahi kwamba kampuni ya Apple imejipanga sawa sawa katika ushindani na makampuni mengine ambayo yako juu na yanatoa huduma hiyo mfano Netflix na Disney Plus.
Hii inadhihirika dhahiri kwa sababu hata idadi ya maonyesho kupitia huduma hiyo ya Apple yameongezeka kwa kiasi kikubwa na kila kukicha huduma hiyo wanaongeza maudhui katika kukuza wigo wao.
Ningependa kusikia kutoka kwako, hebu niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni kweli Apple itaweza ushindani wa makampuni hayo mengine?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.