Apple inaheshimika sana na sera yake ya ulinzi na usalama hasa katika vifaa na huduma zake. Hii imeifanya kampuni kijichukulia sifa nyingi ukiachana na kuaminika.
Kampuni imeweka hili wazi kwa kutoa taarifa hiyo, Kwa haraka haraka kampuni inasema imefanikiwa kuzuia zaidi ya dola bilioni tano kuibwa katika soko lake maarufu la App sababu zikiwa ni ulaghai.

Hili limefanikiwa kutokana na mambo kadhaa kama vile uchambuzi wa App katika soko hilio, sheria ngumu katika App zenye manunuzi ndani yake, njia za kubana za ulipaji na sera nyingine katika soko hilo.
Hapo ni kwenye swala zima la pesa, Pia Apple hawajaishia hapo, wameendelea na kusema kuwa wameweza kuzuia zaidi ya App milioni 1.6 ambazo kwa namna moja au nyingine vingeweza kuwa na udanganyifu kwa wateja.
Apple kupitia AppStore badi inajitahidi kuhakikisha kuwa unazidi kujiboresha katika swala zima la ulinzi, hii ikiwa ni sehemu ya kuwalinda wateja wake.

Licha ya kuwa soko la pili kwa ukubwa kuhusiana na maswala ya App, Kwa usalama limilipita hadi soko la Google maarufu kama Play Store.
Kumbuka mara nyingi taarifa hizi huwa zinatolewa ili kuwahakikishia wateja wapo katika hali gani..kampuni inafanya vitu gnai ili kuhakikisha kuwa wanalindwa.
NIngependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Uwanja Wa Comment, Hili Umelipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.