Apple ni moja kati ya kampuni kubwa sana na mara kwa mara limekua likiweka rekedi nyingi sana katika sekta ya teknolojia.
Kwa mwaka jana pia kampuni ya Apple ilitoa ripoti ya vifaa vyake ambavyo vinatumiwa na wateja wake lakini kwa mwaka huu mpaka kufika sasa kampuni imetoa ripoti ambayo inasema kwa sasa wamefikia bilioni 2.
Vifaa ambayo vimewekwa hapa ni iPhone, iPad, Mac na vifaa vyake vingine vingi, kwa haraharaka namba hii inaonyesha ukuaji wa kasi au ongezeko la kasi la utumiaji wa vifaa kutoka Apple.
Kumbuka mwaka 2016 ndio kwa mara ya kwanza kampuni ilifikisha vifaa bilioni 1 ambavyo vinatumika kwa wateja wake na mwaka 2022 ndio ikapita bilioni 1.5.
Kwa harakaharaka ni kwamba kampuni inaongeza utumiaji wa vifaa vipya –vinavyotumika na wateja— milioni 100-150 tokea mwaka 2019.
Kingine ni kwamba ongezeko hili la bilioni moja mpaka bilioni mbili limetokea kwa kipindi cha miaka saba tuu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unahisi bilioni 3 wataipata mwaka gani? Na pia niambie una vifaa vingapi vya Apple ambavyo unatumia.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.