MacBook ni kompyuta mpakato (Laptop) kutoka Apple ambazo zina maumbo madogo ambayo yanazifanya kuweza kubebeka kwa urahisi.
Ni wazi kwamba mnamo 2008 Steve jobs alikua na uwezo wa kuongezea uwezo wa 3G katika MacBooks lakini hilo lilishindikana baada ya kujua kwamba chip inayohitajika itachukua sehemu kubwa ya jumba la MacBook.
Hivyo basi kwa muda huo wakaachana kabisa na swala zima la 3G katika kompyuta hizo, ni wazi kwamba teknolojia inazidi kuongezeka na mambo mapya yanagunduliwa.
Fikiria kama Apple wakiwa na uwezo wa kuunganisha uwezo wa modem ya bila waya katika chip zake ndogo hizi ambazo zinatumika katika vifaa vyake ili kuweza kukubali uwezo wa 5G.
Wao Apple hili wanaliweka wazi na wanaimani kuwa zoezi zima litatimia mpaka kufikia mwaka 2028 japokua teknolojia hii inaweza ikwa imeshafika miaka mitatu nyuma.
Apple wamedai kuwa miaka hiyo mingine hapo kati wataitumia ili kuhakikisha zoezi hilo wanaliwezesha katika vifaa vyao vya MacBook.
Kumbuka pia MacBook yenye uwezo wa 5G ni ya muhimu sana kwa sasa fikiria kama mtu yoko kwenye eneo ambalo hakuna WiFi, hii itakua na msaada mkubwa sana.
Mara nyingi watumiaji wa MacBook wamekua wakitumia iPhone zao kama chanzo kikubwa cha intaneti katika vifaa hivyo.
Jambo hilo linaenda kupatiwa suluhisho lakini hapa cha kuvumilia ni muda tuu ambao umepangwa – lakini nani anajua bwana, teknolojia inaweza ikakushangaza kwa kuingia katika soko mapema zaidi ya muda tarajiwa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je wewe utakua unatumia MacBook yenye uwezo wa 5G au ni sawa tuu kutumia hotspot ya simu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.