Baada ya kuendelea kupata mafanikio mengi katika iPhone 6 sasa Apple wakuletea MacBook nyembamba zaidi na yenye uzito mdogo zaidi. MacBook hiyo inayoenda kwa jina la ‘MacBook’, bila ‘Air’ wala ‘Pro’ kama tulivyozoea ina uzito wa kilogramu 0.9 na wembamba wa milimita 13, yaani sentimita 1.3.
Laptop hiyo imetambulishwa kwenye mkutano mdogo uliokuwa umeandaliwa na Apple kwa ajili ya kuonesha mambo mengi yanayoweza fanyika kwa kutumia saa yao mpya.
Sifa kuu za laptop hii ni kama ifuatavyo;
i. Kwa wembamba wa sentimita 1.3 imeifanya MacBook hii kuwa nyembamba kwa zaidi ya asilimia 25% ukilinganisha na toleo jembamba la MacBook Air.
ii. Inakioo cha upana wa inchi 12 pia kikiwa na kiwango bora cha muonekano wa Retina na ‘resolution’ ya 2304 x 1440. Apple wanadai kioo hichi kinakula chaji kidogo sana kwa zaidi ya asilimia 30% kikilanganishwa na vioo vinavyotumika kwa sasa.
iii. Mfumo wa CPU unaoiendesha umeondoa ulazima wa kuwa na feni ya kuondoa joto, hivyo usitegemee kelele za feni wala joto sana kwani imetumia teknolojia mpya ya CPU kutoka Intel inayoenda kwa jina la Core M Broadwell CPU. Tazama picha china inayoonesha tofauti ya CPU hii na zile zinazotumika kwa sasa, CPU mpya ni ndogo kwa takribani asilimia 67%.
iv. Pia kuna teknolojia mpya wameitumia katika kibodi zake ambazo wenyewe wanadai ni bora zaidi na imepunguza ata ukubwa mzima wa kibodi katika laptop hiyo.
v. Itakuwa na RAM ya GB 8 na pia uwezo wa betri wa zaidi ya asilimia 34 ukilinganishwa na MacBook za sasa.
vi. Kutakuwa na matoleo mawili, kuna moja la dola 1,299 za kimarekani (Milioni 2.37 za Kitanzania) ina prosesa 1.1 Ghz Core M, na yenye ukubwa wa diski uhifadhi wa GB 256 katika teknolojia ya SSD. Toleo jingine ni la dola 1,599 za kimarekani (Milioni 2.9 za Kitanzania) ina prosesa 1.2 Ghz na ukubwa wa diski uhifadhi wa GB 512 (SSD).
[metaslider id=2801]
Itegemee MacBook hii sokoni ifikapo mwezi wa nne mwaka huu. Kumbuka unaweza kuwasiliana nasi kupitia mhariri (at) teknokona.com au kupitia akaunti zetu za Twitter, Facebook na Instagram .
No Comment! Be the first one.